Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za Filamu Tanzania yashauriwa kutangaza Tasnia ya Filamu kimataifa
Katibu Mtendaji Bodi
ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo (Kulia) akifungua kikao kati ya wajumbe kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na Kamati ya maandalizi
ya Tuzo za TAFA leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara
hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.
Kaimu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel
(kushoto) akizungumza na wadau wa filamu waliofika katika Ofisi za Wizara hiyo
kuwasilisha taarifa ya maandalizi ya Tuzo za TAFA nchini
itakayofanyika
tarehe 23 Mei mwaka huu. Kulia ni Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo
Mwenyekiti wa Kamati
ya Maandalizi ya Tuzo za TAFA Bibi. Caroline Gachara Gul (kulia) akiwasilisha
taarifa ya maandalizi ya Tuzo za TAFA nchini kwa Uongozi wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na watendaji kutoka Bodi ya Filamu nchini
leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa kamati hiyo Bibi. Siima
Rubibira.
Wajumbe kutoka Kamati
ya Maandalizi ya Tuzo za TAFA pamoja na maafisa wanaosimamia Filamu nchini
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakimsikiliza kwa makini
mjumbe aliyekua akichangia (hayupo pichani) wakati wa kuwasilisha taarifa ya
maandalizi ya Tuzo hizo kwa uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo.
Rais wa Shirikisho la
Filamu Tanzania Bw. Saimon Mwakifwamba (kushoto) akichangia wakati wa kuwasilisha
taarifa ya maandalizi ya Tuzo za TAFA nchini kwa
uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na watendaji
kutoka Bodi ya Filamu nchini leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni mjumbe wa
kamati hiyo Bw. John Kalage.
Kaimu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Mchezo Prof. Elisante Ole Gabriel
(waliokaa katikati), Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Prof Elimas Mwansoko (wapili
kushoto), na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo (wapili kulia)
katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za TAFA na
watendaji wanaosimamia shughuli za filamu nchini. Picha
na: Genofeva Matemu - Maelezo.
No comments:
Post a Comment