LESENI ZA WACHIMBAJI MADINI 3,449 ZATOLEWA
Na Greyson Mwase
Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava
amesema kuwa jumla ya leseni 3,449 zilitolewa katika mwaka wa fedha
2014/15 kwa wachimbaji wa madini ya aina mbalimbali nchini.
Mhandisi Mwihava aliyasema hayo wakati akielezea mafanikio ya sekta za nishati na madini kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini uliofanyika katika hoteli ya Kunduchi Beach iliyopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam unaoendelea.

Lengo
la mkutano huo ni kujadili mafanikio na changamoto katika utekelezaji
wa majukumu ya Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Tasisi zake.
Alisema
kati ya leseni hizo leseni mbili ni za uchimbaji mkubwa, leseni za
utafutaji wa madini ni 694, leseni za uchimbaji wa kati ni 21 na leseni
za uchimbaji mdogo ni 2,732.
Mhandisi
Mwihava alieleza kuwa lengo la kutoa leseni hizo ni kuhakikisha kuwa
wachimbaji wanaendesha shughuli za uchimbaji katika maeneo rasmi
yaliyopimwa na kuongeza pato la serikali.
Alisema
mbali na utoaji wa leseni hizo, wamiliki wa leseni 1,144 wa leseni za
utafutaji madini, wamiliki 34 wa leseni za uchimbaji mkubwa na wamiliki
83 wa leseni za uchimbaji mdogo walisajiliwa kutumia mfumo wa huduma za
leseni kwa njia ya mtandao ujulikanao kama Mining Cadastre Portal.
Alisema kuwa mfumo huo unawezesha wamiliki wa migodi hiyo kuhuisha leseni kwa kutumia mtandao badala ya kufunga safari hadi kwenye ofisi za madini.
Alisema kuwa mfumo huo unawezesha wamiliki wa migodi hiyo kuhuisha leseni kwa kutumia mtandao badala ya kufunga safari hadi kwenye ofisi za madini.
Mhandisi
Mwihava akielezea mafanikio mengine katika sekta ya madini alisema kuwa
mwezi Desemba, 2014 kampuni ya uchimbaji madini ya Resolute (T) Limited
ilikabidhi miundombinu yote ya mgodi wa Golden Pride kwa Chuo cha
Madini Dodoma ambayo itatumia kufundishia wanafunzi wa chuo hicho kwa
vitendo. Aliongeza
kuwa mafanikio mengine ni pamoja na uanzishwaji wa Ofisi mbili za Kanda
na nne za Afisa Madini Mkazi ambazo zinafanya kazi.
Alitaja
ofisi hizo kuwa ni pamoja na Kanda ya Ziwa Nyasa – Songea, Kanda ya
Ziwa Viktoria Mashariki – Musoma, Ofisi za Madini Mkazi zilizopo
Bariadi, Moshi, Nachingwea na Njombe. Wakati
huo huo akielezea mafanikio ya sekta ya nishati, Mhandisi Mwihava
alisema kuwa hadi kufikia mwezi Februari mwaka huu, utekelezaji wa mradi
wa Kinyerezi 1 ulikamilika kwa asilimia 84 ambapo mitambo yote minne
pamoja na mitambo ya kupooza injini imeshafungwa kwenye eno la mradi na
kusisitiza kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika mapema Juni mwaka huu.
Aliongeza
kuwa mradi wa ujenzi wa bomba la gesi umekamilika kwa asilimia 97 na
kuongeza kuwa mara baada ya ukamilishwaji wake wananchi wataanza kupata
umeme wa uhakika na kwa gharama nafuu.
“ Pamoja na hayo, hadi kufikia Februari, 2015 jumla ya wateja wapya 131, 180 walio ndani na nje ya gridi ya taifa wameunganishwa na umeme ambayo ni sawa na asilimia 75 ya lengo la Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kwa mwaka ambalo ni kuunganisha wateja 175,000. “ Alisisitiza Mhandisi Mwihava.

mafanikio mengine kuwa ni pamoja na uanzishwaji wa kampuni ya maendeleo
ya joto-ardhi Tanzania ambayo ilianza kazi yake rasmi tangu Julai, 2014
na ukamilishwaji wa rasimu ya sera ya nishati na mafuta ambazo ziko
kwenye hatua ya kuwasilishwa kwenye baraza la Mawaziri.
No comments:
Post a Comment