WAZIRI LUKUVI AFUNGUA NYUMBA ZA NHC MRARA BABATI

Sehemu
ya nyumba 40 za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati
mkoani Manyara ambazo zilifumguliwa rasmi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi.
.....................................
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi
amehitimisha ziara yake ya kutatua migogoro ya Ardhi katika mikoa ya
Mwanza, Arusha na Manyara na ameweza pia kuweka jiwe la msingi mradi wa
nyumba za gharama nafuu Buswelu Mwanza na kufungua nyumba za aina hiyo
zilizojengwa na NHC katika eneo la Longido Arusha na Mrara Babati. Picha
za ufunguzi wa Mradi wa Mrara na Muungano Saguya-Babati

Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akitoa maelekezo kwa watendaji
wake muda mfupi kabla ya ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu
zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati mkoani Manyara


Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akionyeshwa mipaka ya eneo
linalomilikiwa na NHC na Msimamizi wa Mradi wa NHC Mrara Babati Bi Linda
Kasilima baada Mkurugenzi Mkuu kubaini kuwepo kwa uvamizi wa baadhi ya
viwanja vya Shirika. Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.
Joel Bendera ameagiza wote waliovamia viwanja hivyo kunyang’anywa mara
moja na nyumba zao kuvunjwa bila fidia.

Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akimpokea Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi alipowasili
katika mradi wa nyumba za gharama nafuu unaotekelezwa na NHC ambapo
aliifungua rasmi baada ya kukamilika. Nyjmba hizo 40 sasa zinauzwa kwa
wananchi mbalimbali wa Babati na nje ya Wilaya hiyo wanaohitaji.
No comments:
Post a Comment