Mrisho
Mpoto akimkabidhi kifaa cha kupimia magari mmoja wa wakazi wa Dodoma
Beatrice Chilewa (kulia), muda mfupi baada ya kujishindia moja ya swali
lililoulizwa na msemaji wa GS1, Pius Mikongoti, ambalo lilikuwa
likimtaka ataje nchi tatu za Kusini mwa Jangwa la Sahara zinazotoa
Barcode na namba za utambulisho wa nchi hizo, wa kwanza kutoka kushoto
ni Mkurugenzi wa kampuni ya Josekazi Auto Garage ambaye ndiye mmiliki wa
kifaa hicho cha kupimia magari.
MKURUGENZI
wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba,(wanne
kushoto) akiongea na baaddhi ya wakazi wa Dodoma mjini (hawapo pichani)
waliohudhuria Semina ya Kamata Fursa ndani ya Ukumbi wa Royal Village
mapema jana,ambapo aliwaeleza wakazi hao namna ya kuwapatia mbinu
mbalimbali za kujikwamua kupitia rasilimali zilizopo ndani ya mkoa huo
wa Dodoma.
Msemaji
kutoka GS1, Pius Mikongoti akiwalezea wakzi wa Dodoma namna ya
kunufaika kupitia huduma zitolewazo na GS1, hasa katika mfumo wa kutumia
Barcode.
Msanii
wa kughani Mashairi Mrisho Mpoto akiwapa historia yake ya mafanikio na
namna alivyoweza kutumia fursa hadi kufikia hapo alipo kwa sasa.
Afisa
Utekelezaji na mipango wa NSSF Ally Mkulemba akitoa semina kwa wakazi
wa Dodoma, huku akiwapa mbinu za kutumia fursa katika kusongesha
mafanikio kupitia mikopo mbalimbali itolewayo na Shirika hilo mapema
jana ndani ya Ukumbi wa Royal Village.
Sehemu
ya watu waliojitokeza kwenye Semina ya Kamata Fursa iliyokuwa
ikifanyika ndani ya Ukumbi wa Royal Village,mjini Dodoma hapo jana.
No comments:
Post a Comment