Header Ads

MPINA KUENZI UTAMADUNI WA WASUKUMA.

Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoani Simiyu, waliofika eneo hilo kushuhudia mpambano ulioandaliwa na mbunge huyo wa ngoma za asili ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
MBUNGE wa Jimbo la Kisesa(CCM), Luhaga Mpina ameahidi kuendelea kuenzi utamaduni wa ngoma za kabila la wasukuma kwani zimekuwa ni sehemu ya kuimarisha mshikamano miongoni mwa jamii hiyo.

Mpina alitoa kauli hiyo juzi wakati akifunga mpambano wa ngoma za asili katika Kijiji cha Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoani Simiyu uliwakutanisha Malogi Hamsini Mgika na Magise Jilunga Mgalu.

Hata hivyo katika mpambano huo ulihudhuriwa na watazamaji zaidi elfu nane kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Simiyu ambapo Magise Jilunga aliibuka mshindi baada ya kumbwaga Malogi.

Akizungumza mara baada ya mpambano huo, Malogi Hamsini alikubali kushindwa na mpinzani wake na kueleza kuridhika na uamuzi uliofanywa na kuomba kukutanishwa tena siku nyingine na mpinzani wake huyo.

Naye Magisa Jilunga alisema pamoja na kumshinda mpinzani wake lakini alikiri pambano hilo lilikuwa gumu kwake na kuamba nae pia kurudiana ombi ambalo lilikubaliwa na Mbunge wa jimbo hilo.

Pambano hilo lililodhaminiwa na Mbunge Mpina lilivuta hisia za mashabiki wengi na kuomba kufanyika mara kwa mara kwa pambano hilo kwani linaleta umoja na mshikamano miongoni mwa jamii.

Mpina aliwazawadia shilingi milioni moja kila mmoja katika mpambano huo na kuahidi kudhamini tena pambano lingine kama hilo baadae mwakani. ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA YALIYOJIRI.

No comments:

Powered by Blogger.