BENKI YA KIARABU YA MAENDELEO YA UCHUMI YA AFRIKA ( BADEA)YATOA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 12.0 (SHILINGI BILIONI 20.1) KUSAIDIA MAENDELEO KATIKA WILAYA YA SAME NA MWANGA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu
wa serikali Dr.
Servacius Likwelile akiwa na ujumbe kutoka Tanzania wakiwa tayari kutiliana
saini mkataba wa makubaliano ya mradi wa maji katika Wilaya ya Same na Mwanga.
Aliye kushoto kwake ni Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa
Mwenyekiti na Mkurugenzi Msimamizi wa
mfuko wa maendeleo wa Saudia.Fedha hizo zimetoka BADEA.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr.
Servacius Likwelile akitia saini
makubaliano ya mradi wa maji katika Wilaya ya Same na Mwanga. Aliye kushoto
kwake ni Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo
wa Saudia. Aliyeko kulia ni Bi. Suzan Mkapa, Mkurugenzi wa sheria kutoka Wizara
ya Fedha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu
wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Msimamizi wa
mfuko wa maendeleo wa Saudia, wakibadilishana mikataba hiyo baada ya kutiliana
saini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu
wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Msimamizi wa
mfuko wa maendeleo wa Saudia, wakiionyesha mikataba hiyo kwa waliohudhuria
sherehe hiyo baada ya kutiliana saini.
======== ======= ========
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius
Likwelile, mchana wa leo ametiliana saini makubaliano ya mkataba wa
kuanzisha Mradi wa Maji katika Wilaya ya Same na Mwanga mkoani
Kilimanjaro.
Dr.
Likwelile alisaini Mkataba huo kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya uchumi ya
Afrika. Aliye wakilisha Benki hiyo ni Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni
Makamu wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa
Saudia.
Aidha
katika kutiliana saini Mkataba huo Dr. Likwelile alimueleza Eng. Yousef
I. Al-Bassam kuwa Serikali ya Tanzania inatambua kuwa BADEA imetoa
Dola za Kimarekani milioni 12.0 sawa na shilingi Bilioni 20.1 za
Kitanzania kwa ajili ya kusaidia mradi wa maji katika Wilaya ya Same na
Mwanga.
Hivyo
inatoa shukrani zake za dhati kwa BADEA kwa kusaidia kuchochea
maendeleo ya Tanzania.
“Msaada huu tulioupata leo utaisaidia Serikali kutatua tatizo la maji
katika wilaya ya Same na Mwanga, hii inaonyesha ni jinsi BADEA unaunga
mkono na kutekeleza jukumu zima la kushiriki katika masuala ya kijamii
na ya kiuchumi kwa nchi yetu ya Tanzania, hivyo tunaomba muendelee
kutusaidia”. Alisema Dr. Likwelile.
Dr.
Likwelile alimueleza Eng. Yousef I. Al-Bassam kuwa, kama anavyofahamu
gharama za mapendekezo ya mradi mzima ni Dola za Kimarekani million
110.43 na hii inahitaji uchangiaji kutoka katika mifuko mingine kama
mfuko wa maendeleo wa Saudia , Mfuko wa Kimataifa wa OPEC na Serikali
kuchangia fedha kusaidia mradi huu.
"Kwa
hili sina wasiwasi nalo kwani ninafuraha kujua kwamba umeshakubaliana
na ninaujasiri kuwa jitihada zako zitafanikiwa. Mradi huu wa maji wq
wilaya ya Same na Mwanga unalenga kusaidia kuwepo kwa maji kwenye jamii
mbalimbali zilizopo kwenye mradi huo.” Aliongeza Dr.Likwelile.
Aliendelea kusema kuwa,mradi huo utakapo kamilika:
(i) utaongeza kiwango cha watu wengi kuweza kupata maji safi na salama ya kunywa.
(ii)
Uchumi wa Same na Mwanga utaimarika pamoja na hali ya afya kwa jamii
nayo itakuwa imara hasa kwa maeneo yale yanayoguswa na mradi.
(iii) Hali ya maisha ya watu wa Same na Mwanga itainuka.
“Mafanikio
ya ukamilishaji wa mradi huu ni muhimu sana kwa uchumi wa jamii na
maisha bora kwa watu wa wilaya ya Same na Mwanga”. Alisema Likwelile.
Dr. Likwelilie alimalizia kwa kusema kuwa“Tanzania na Saudia ni marafiki
wa muda mrefu sana, hivyo tutazidi kushirikiana na kuhakikisha kila
kitu kinaenda sawa”.
Imetolewa na:
Ingiahedi Mduma
Msemaji - Wizara ya Fedha
Washington D.C
No comments:
Post a Comment