Header Ads

WASOMI SONGEA WAMTAJA ABATE LAMBERT KUWA MWANAHISTORIA WA KARNE YA 21



 Abate mstaafu wa Abasia ya Peramiho Jimbo kuu katoliki la Songea Lambert Doerr OSB katikati wa kati akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa Waumini wa Parokia ya Mbingamharule Wilayani Songea Mkoani Ruvuma,kama sehemu ya kumpongeza baada ya kutimiza miaka 50 ya Umisionari hapa Nchini.

Waumini wa Parokia ya Mbingamharule Jimbo kuu katoliki la Songea mkoani Ruvuma,wakifuatilia kwa makini adhimisho la misa Takatifu ya shukurani ya kutimiza miaka 50 ya Umisionari ya Abate mstaafu wa Abasia ya Peramiho LambeDoerr hapa Nchini.(PICHA NA JULIUS KONALA) 
-----------------
Na Julius Konala wa demasho.com,Songea
BAADHI ya Wasomi mkoani Ruvuma,wamemtaja Abate mstaafu Lambert Doerr OSB wa Abasia ya Peramiho kuwa ni Mwanahistoria wa karne ya 21 kutokana na mchango wake mkubwa wa kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo hapa Nchini ikiwemo katika nyanja ya Elimu.

Matamko hayo yalitolewa na Wasomi hao kwa nyakati tofauti wakati walipokuwa wakitoa mada mbalimbali katika kongamano lililoandaliwa kwa ajili ya kuzungumzia juu ya maisha na kazi zilizofanywa na Abate huyo katika kipindi chake cha miaka 50 ya Umisionari hapa Nchini lililofanyika kwenye ukumbi wa Nyerere chuo kikuu cha Sauti tawi la Songea.

Akitoa mada katika kongamano hilo Padre Dr.Xsaver Komba,alisema kuwa moja ya mchango wa uliotolewa na Abate Lambert wakati akiwa Mwalimu bora na mwadilifu katika Seminari ndogo ya Likonde na Seminari kuu ya Peramiho alifundisha kwabidii kwa kufuata misingi ya ualimu iliyopelekea  kutoa wasomi wengi ambao miongoni mwao ni viongozi wakubwa wa Serikali na Dini.

Alisema kuwa michango mingine aliyoitoa ni pamoja kuwaunganisha Waafrika kuwa kitu kimoja na wazungu kwenye nyumba za kitawa, kuwasomesha baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mbinga Mharule kwa kuwalipia ada ya shule,kusogeza huduma ya maji safi na salama kwa kilometa saba,kujenga zahanati,ujenzi wa barabara ya Lambert yenye urefu wa kilometa tatu,kusaidia wazee wasiojiweza,watoto Yatima pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya dini ya kikristu na waislamu.

Alisema kuwa maadhimisho hayo ya Jubilei ya miaka 50 ya Umisionari Nchini yatakwenda sambamba na na uanzishwaji wa chuo cha ufundi cha Mtakatifu Lambert mjini hapa kitakachotoa fani ya kompyuta,ushonaji na uselemala kama sehemu ya kumuenzi.

Naye mmoja wa watoa mada na mwanafunzi  aliyefundishwa na Abate huyo,Dr.Damas Mbogoro ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali hapa Nchini alimwelezea Abate Lambert kuwa ni mtu  ambaye hakuwa mchoyo wa elimu na kudai kwamba alikuwa karibu na watu katika kusikiliza shida na matatizo yao.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika kongamano hilo,Padre Dastan Mbano ambaye alimwakilisha Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Songea Damian Dallu,alisema kuwa Abate Lambert ni hazina kubwa sio kwa upande wa kanisa peke yake bali ni kwa jamii nzima.

Mbano alisema kuwa kazi nzuri na kumbukumbu za Abate huyo zinapaswa kutangazwa,kuenziwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya faida ya vizazi vijavyo huku mwakilishi wa Baraza la mila kasian Shauritanga,alisema kuwa wamisionari Wabenediktini wa Abasia ya Peramiho watakumbukwa kwa mchango wao wa kusaidia kutunza kumbukumbu za mila na desturi za wangoni katika makumbusho ya vita ya majimaji na kuupatia mkoa na taifa kwa ujumla sifa pekee ya utunzaji.

1 comment:

Mbele said...

Shukrani kwa taarifa. Mimi ni mmoja wa wanafunzi wa Mhashamu Abate Lambert, wakati nasoma seminari ya Likonde, 1967-1970.

Alitufundisha ki-Ingereza na Historia. Hungeweza kumkutapopote asiwe na kitabu anakisoma. Akiena matembezi, kwenye maeneo ya mashamba ya shule, utamkuta anasoma kitabu

Alituhamasisha kuwa wasomaji sana wa vitabu. Vile vile, alituhamasisha kuwa watafiti katika historia kwenye maeneo tulikotoka. Tulijifunza mengi katika kuongea na wazee na kurekodi masimulizi yao, na pale shuleni Abate Lambert alituongoza katika kuchapisha jarida liloitwa "Our Past"

Namshukuru sana kwa elimu aliyonipa, na mfano wa kuwa msomaji asiyechoka.

Powered by Blogger.