Vijana washauriwa kujiajiri katika sekta ya Sanaa

Spika
wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa
(Kulia) akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa
wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi
ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza
bidhaa zao wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
waliotembelea Taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.

Mmoja
wa wabunge wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Susan
Nakawuki (mwenye blauzi ya pinki) akinunua bidhaa kutoka kwa mmoja wa
wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi
ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza
bidhaa zao wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
waliotembelea Taasisi hiyo jana.

:
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella
Mukangara (MB) akiweka saini katika daftari la wageni katika moja ya
kikundi cha wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi
ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza
bidhaa zao kwa wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
waliotembelea Taasisi hiyo jana.

Baadhi ya Wabunge wa Afrika Mashariki akiwemo Mhe. Shyrose Bhanji anayewakilisha Tanzania
katika bunge hilo wakiangali kazi za sanaa ya uchingaji kutoka kwa
mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi
ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza
bidhaa zao kwa wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
waliotembelea Taasisi hiyo jana.

Mbunge
wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Shyrose Bhanji wa Tanzania
akimkabidhi zawadi ya sinia lililotokana na kazi za uchongaji Spika wa
Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Margareth Zziwa mara baada ya kupenda
bidhaa hiyo na kuamua kumnunulia spika huyo jana wilayani Bagamoyo
wakati wa ziara ya Wabunge wa Afrika Mashariki katika Taasisi ya Sanaa
na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa).

Katikati
ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki ambaye pia ni mtoto wa Baba wa
Taifa Mhe. Makongoro Nyerere (katikati) akifurahia jambo na Katibu Mkuu
wa Wizara ya Afika Mashariki wa Serikali ya Tanzania Bibi. Joyce
Mapunjo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel walipokuta katika viwanja vya Taasisi
ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) wakati wa ziara ya wabunge wa
Afrika Mashariki katika Taasisi hiyo. Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari.Vijana, Utamaduni na Michezo.
No comments:
Post a Comment