SHIMIWI YATAKA VILABU VITAKAVYOSHIRIKI KUJISAJILI MAPEMA
Mwenyekiti
wa SHIMIWI Taifa Bw. Ally Katembo akifungua mkutano maalumu wa kupanga
ratiba ya Mashindano ya SHIMIWI uliofanyika katika ukumbi wa Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam mapema leo.
Kushoto kwake ni Katibu wa SHIMIWI Bw. Moshi Makuka (wa pili) na wajumbe
wa SHIMIWI wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa.
Katibu
wa SHIMIWI Bw.Moshi Makuka (wa pili kutoka kushoto) akitoa mada wakati
wa mkutano maalumu wa kupanga ratiba ya timu zitakazoshiriki kwenye
SHIMIWI mwaka huu katika ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora jijini Dar es Salaam mapema leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa SHIMIWI
Taifa Bw. Ally Katembo na wengine ni wajumbe wa SHIMIWI Taifa
wakifuatilia mada.
Mmoja wa Wajumbe wa SHIMIWI akishiriki katika zoezi la kupanga makundi mbalimbali katika ratiba ya michezo ya SHIMIWI.
Kamati
maalumu ikipanga ratiba ya makundi mbalimbali katika michezo ya mpira
wa miguu,mpira wa pete, bao,karata, riadha,kuvuta kamba na kurusha tufe
katika michezo ya SHIMIWI.
Baadhi ya wajumbe wa SHIMIWI na Viongozi wa Vilabu vya Michezo wakifuatilia mada.
======= ======== ======
Viongozi
wa vilabu vya timu zinazotarajia kushiriki kwenye Mashindano ya
Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI)
yanayotarajiwa kuanza Septemba 27 mjini Morogoro wametakiwa kusajili
timu zao mapema ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza hapo baadae wa
kushindwa kusajiliwa kutokana na mapungufu ya timu zao.
Mwenyekiti
wa SHIMIWI Taifa Bw. Ally Katembo aliyasema hayo alipokuwa akifungua
mkutano maalumu wa kupanga ratiba ya mashindano ya SHIMIWI uliofanyika
ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam
mapema leo.
Bw.Katembo
alizitaka timu zinazotumia wachezaji walioajiriwa kwa mkataba wa miezi
mitatu kuacha tabia hiyo na badala yake watumie wachezaji wenye mikataba
ya mwaka mmoja na kuendelea ili kuepuka tatizo la kutumia mamluki
kwenye timu zao.
"Tafuteni
wachezaji ambao ni wafanyakazi katika Ofisi nyingine za Serikali kama
timu zenu zina mapungufu ya wachezaji" alisema Bw. Katembo.
Naye
Katibu wa SHIMIWI Bw.Moshi Makuka aliwataka viongozi hao kutoa taarifa
ya timu ambazo hazitashiriki mashindano hayo mapema iwezekanavyo ili
kuepuka gharama zinazotumika katika maandalizi ya timu zao.
"Timu
ambazo hazitaweza kushiriki ziwe wazi kusema hazishiriki kwa sababu
SHIMIWI inatumia gharama nyingi kwenye maandalizi" alisema Bw.Makuka.
Mkutano
huo ulihudhuriwa na wajumbe wa SHIMIWI na viongozi wa vilabu vya timu
mbalimbali kutoka katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za
Serikali, Sekretarieti za Mikoa, Mashirika ya Umma na Halmashauri za
Wilaya.
No comments:
Post a Comment