KIKWETE AMVALISHA CHILIGATI ‘KIATU’ CHA MAKINDA…!

Capt. John Chiligati ambaye ni Mwenyekiti mpya wa Kamati mpya ya Uongozi wa Mkurabita
“NIMSHUKURU Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dk. Jakaya Kikwete kwa kuniona na kuniamini na hivyo, kuniteua ili
niweze nami kuvaa kiatu anachokiacha Mheshimiwa makinda”. Anasema,
Kapteni Mstaafu wa John Chiligati ambaye ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika hafla
ya uzinduzi wa Kamati mpya ya Uongozi wa Mpango wa Kuratibu na
Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) na
kuwapongeza wajumbe wa Kamati hiyo waliomaliza muda wao.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Dar es Salaam
Serena jijini Dar es Salaam, Chiligati ambaye ameteuliwa na Rais Kikwete
hivi karibuni kuwa Mwenyekiti wa Kamati mpya ya Uongozi ya Mkurabita
akichukua nafasi iliyotumikiwa kwa takriban miaka 10 na Spika wa Bunge
la Tanzania, Anne Makinda, akasisitiza, “Kwa mtazamo tu wa haraka, kiatu
hiki ni kikubwa kweli kweli, lakini naamini kwa ushirikiano kutoka kwa
wajumbe wenzangu, watendaji wa Mkurabita, Waziri na Ikulu yote pamoja na
wadau wote na wapenda maendeleo, tutaweza kutekeleza kazi hii kwa
ushindi mkubwa.”
Anaongeza, “Hii ni kwa kuwa kweli nimeona nia thabiti ya
Serikali ya kutaka kuinua uchumi wa nchi yetu kupitia rasilimali ardhi
na biashara halali zinazoendeshwa na Watanzania…” Mwenyekiti huyo
(Chiligati) alisema katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Kamati mpya kuwa,
endapo Mkurabita utaeleweka zaidi kwa umma na malengo yake kutekelezwa
ipasavyo, uchumi wa nchi utaimarika. Akasema, “Naomba Mungu atusaidie
mimi na wenzangu ili nia hii ya kusisimua uchumi wa nchi yetu kupitia
urasimishaji iweze kuwa ya kweli.”

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mkurabita aliyemaliza muda wake, Anna Makinda.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mkurabita
inayomaliza muda wake, Anne Makinda akasema lengo la Serikali kuanzisha
Mkurabita ni kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kutumia rasilimali na
biashara zao ambazo ni rasmi. Akasema, “Mkurabita imepewa wajibu wa
kuhakikisjha rasilimali na biashara zinazoendeshwa nje ya mfumo
unaotambulika kisheria zinakuwa rasmi na hivyo, kutambulika kisheria.”
“Matokeo ya tathmini ya sekta isiyo rasmi iliyofanywa na
mtaalamu kati ya mwaka 2004 na 2005 yalionesha kuwa, asilimia 89 ya
ardhi na asilimia 98 ya biashara hazikidhi matakwa ya kisheria. Thamani
ya rasilimali hizi ni jumla ya Dola za Kimarekani bilioni 29. 3
alizozitaja kuwa ni mtaji mfu.”
Kwa mantiki hiyo, Makinda alisema kazi ya kurasimisha rasilimali hizo inategemewa kufufua mtaji huo mfu na kuufanya kuwa mtaji hai utakaochangia kikamilifu ukuaji wa uchumi wa taifa
Kwa mantiki hiyo, Makinda alisema kazi ya kurasimisha rasilimali hizo inategemewa kufufua mtaji huo mfu na kuufanya kuwa mtaji hai utakaochangia kikamilifu ukuaji wa uchumi wa taifa
No comments:
Post a Comment