Header Ads

Rais Kikwete atawazwa kuwa chifu msaidizi wa waluguru na chifu kingalu huko kinole, morogoro, apewa jina la Chidukila


 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumtawaza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.  Rais Kikwete pia alipewa jina la CHIDUKILA, lenye kumaanisha "muibukaji", kwa maana ya kwamba Rais Kikwete ana uhuru wa kuibuka kijijini Kinole bila taarifa wala kusubiri kualikwa.

 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumvika mgolole Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014
 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimvika  mgolole Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo
 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimvipa pama lililosukwa kwa ukindu  Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo

No comments:

Powered by Blogger.