CHRISTIANO RONALDO ATWAA TUZO YA MWANASOKA BORA BARANI ULAYA 2013 – 2014
Mpachika
mabao hatari wa kimataifa, Cristiano Ronaldo amefanikiwa kutwaa Tuzo
ya mwanasoka bora barani ulaya ”UEFA Best Player ” kwa mwaka 2013 na
2014 baada ya kuisaidia klabu yake ya Real Madrid kutwaa kombe la ligi
ya mabingwa.
Ronaldo amewabwaga wachezaji wenzake waliokuwa katika
kinyang’anyiro hicho akiwemo Straika wa Bayern Munich Arjen Robben na
goli kipa Manuel Neuer Katika kura zilizopigwa wazi na waandishi wa
habari wapatao 54.
No comments:
Post a Comment