Ukraine:Kudunguliwa kwa ndege ni uhalifu

Waziri mkuu wa Ukraine Arseniy Yatsenyuk
Waziri
mkuu wa Ukraine Arseniy Yatsenyuk amesema kuwa kudunguliwa kwa ndege ya
Malaysia ni uhalifu wa kimataifa unaopaswa kupelelezwa na mahakama ya
jinai iliyoko The Hague.
Waziri
huyo mkuu amesema kuwa mauwaji hayo yametekelezwa na Serikali ya Urusi,
huku Rais wa Urusi, Vladimir Putin, akirushia lawama Ukraine.
Naye
Waziri mkuu wa Australia Tony Abbott amesema kuwa ajali hiyo ya ndege
ilionekana kuwa tendo la Ugaidi, kwani inaonekana ilishambuliwa na waasi
wanaofadhiliwa na Urusi.
Waziri
mkuu wa Uholanzi Mark Rutte amesema nchi yake inaomboleza vifo vya
zaidi ya watu 150, raia wa taifa lake walioangamia katika ajali ya ndege
ya Malaysia iliyodunguliwa Nchini Ukraine.

Lawama zimekuwa zikirushwa kati ya Ukraine na Urusi
Anasema kuwa kulikuwa na waholanzi 154 kwenye ndege hiyo.
Kati
ya walioabiri ndege hiyo, kulikuwemo takriban watafiti 100 wa ugonjwa wa
ukimwi, wafanyikazi katika idara ya afya na wanaharakati waliokuwa
wanasafiri ughaibuni kuhudhuria mkutano wa kimataifa huko Melbourne.
Aliyekuwa
rais wa Jamii ya Kimataifa inayoshughulikia maswala ya ugonjwa wa
Ukimwi, Joep Lange anadhaniwa kuwa mmoja wa walioabiri ndege hiyo.Chanzo
BBC Swahili
No comments:
Post a Comment