Ndege yatua barabarani Uganda

Ndege hii ilikuwa inaelekea mjini Juba Sudan Kusini
Shughuli ziliathirika leo wilayani Mityana baada ya ndege kutua kwa dharura katika barabara ya magari ya Mityana.
Ndege
hiyo N604AR, iliyokuwa imewabeba wanajeshi wa Marekani, ilitua katika
eneo la Kiwawu umbali wa kilomita 22 kutoka wilaya ya Mityana.
Kwa
mujibu wa mtandao wa Nation, kamishna wa wilaya Joel Walusimbi,
alithibitisha tukio hilo akisema rubani wa ndege hiyo alilazimika kutua
katikati ya barabara
Polisi walisema kuwa ndege hiyo ilikuwa inaelekea mjini Juba Sudan Kusini kutoka uwanja wa ndege wa Entebbe.
No comments:
Post a Comment