NAIBU WAZIRI ANGELLAH JASMINI KAIRUKI ZIARANI DAR ES SALAAM KUANZIA KESHO JULAI 14-18, 2014
Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Jasmine Kairuki (MB) anatarajia
kufanya ziara ya kikazi ya siku tano kuanzia Jumatatu, Julai 14 hadi
Ijumaa 18, 2014 katika jiji la Dar Es Salaam akitembelea asasi
mbalimbali zinazotoa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi kwa lengo
la kujionea huduma zinazotolewa na asasi hizi ikiwa ni pamoja na
kukutana na wananchi wanaopata huduma hii.
Pamoja
na kujionea huduma hizi Mh. Naibu Waziri anatarajiwa kujionea ufanisi
wa kazi zinazofanywa na asasi hizi, changamoto zinazowakabili pamoja na
kupokea maoni, ushauri na kubadilishana mawazo ili kujua jinsi ambavyo
serikali inaweza kuboresha utoaji wa huduma hii.
Katika
ziara hiyo, Mhe. Kairuki anatarajia kutembelea jumla ya asasi 13 ikiwa
ni pamoja na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Taasisi ya Haki za
Binadamu na Mazingira (Envirocare), Kamati ya Msaada wa Kisheria ya Chuo
Kikuu cha Dar Es Salaam na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo
Nyingine ni pamoja na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),
Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC) na Kituo
Kinachoshughulikia Maslahi ya Wanawake na Watoto (TWCWC).
Taasisi
nyingine atazozitembelea ni Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wajane na
Watoto (CWCA), Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Kituo
cha Msaada wa Kisheria cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Nyumba
ya Amani na Ofisi ya Mfuko wa Huduma za Kisheria (Legal Services
Facility).
Mheshimiwa
Kairuki anatarajia kumaliza ziara yake siku ya Ijumaa, Julai 18, 2014
kwa kutembelea Sekretariati ya Msaada wa Kisheria Tanzania ijnayoratibu
shughuli za utaoji wa Msaada wa Kisheria Tanzania na kisha kufanya
mkutano wa majumuisho na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano
wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria kuanzia saa 5:00 asubuhi.
Imetolewa na Wizara ya Katiba na Sheria,
Dar es Salaam,
Jumapili, Julai 13, 2014

No comments:
Post a Comment