MKE WA MBUNGE WA CHALINZE AGAWA MISAADA KWA FAMILIA ZENYE MAHITAJI MUHIMU CHALINZE
Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete,Bi. Arafa Mohammed (kushoto)
akimkabidhi zawadi ya Vyombo vya ndani na Tende mzee Said Khamis Mnyika
wa kijiji cha Changarikwa kata ya Mbwewe kama zawadi ya mbunge huyo
katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan kwa familia zenye mahitaji muhimu
kutokana na kuishi katika mazingira magumu.ambapo vifaa vya ndani pamoja na Tende zitatolewa kwa familia zipatazo 600 katika kata zote za jimbo hilo.
Huu ni mwendelezo wa shughuli za mbunge huyo katika kuwatumikia wapiga kura wake na kuboresha maisha yao ikiwa ni mikakati yake ya kufikia malengo aliyojipangia kwa kushirikiana na wananchi wa jimbo la Chalinze, Kulia ni Mzee Ahmad Ramadhan mmoja wa wazee wa kijiji cha Changarikwa akingoja kukabidhiwa zawadi zake .(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MBWEWE-CHALINZE)
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete(kushoto) akimkabidhi zawadi ya vyombo vya ndani na Tende Mzee Ahmad Ramadhan mmoja wa wazee wa kijiji cha Changarikwa wakati alipotoa zawadi hizo kwa familia zenye mahitaji muhimu katika kata ya Mbwewe jana.
Arafa Mohammed Mke wa Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi zawadi hizo Bi.Halima Hassan katika kijiji cha Changarikwa jana.




No comments:
Post a Comment