MIROSLAV KLOSE AWEKA HISTORIA KOMBE LA DUNIA
Miroslav Josef Klose akishangilia baada ya kutupia bao la pili kwa Ujerumani usiku huu na kuvunja rekodi ya kupachika mabao.
MSHAMBULIAJI
wa Ujerumani na timu ya Lazio ya Italia, Miroslav Josef Klose, ameweka
historia usiku huu baada ya kutupia bao lake la 16 na kuwa mfungaji wa
mabao mengi katika michuano ya Kombe la Dunia iliyoanza mwaka 1930
ambayo kwa sasa inaendelea nchini Brazil.
Klose
ameifungia Ujerumani bao la pili wakati ikitoa kichapo cha mabao 7-1
dhidi ya Brazil katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2014.
Klose
alifunga mabao matano katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2002 na
2006, akatupia manne huko Afrika Kusini mwaka 2010 na mpaka sasa huko
Brazil tayari amefunga mabao mawili moja dhidi ya timu yake na Ghana
wakati la pili dhidi ya Brazil leo.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 36 amempiku mshambuliaji wa Brazil, Ronaldo Luís Nazário de Lima aliyekuwa na mabao 15.
Wachezaji
wengine waliowahi kufunga mabao zaidi ya 11 kwenye michuano hiyo ni:
Gerd Muller wa Ujerumani 14, Just Fontaine wa Ufaransa 13, Pele wa
Brazil 12, Jurgen Klinsmann wa Ujerumani 11 na Sandor Kocsis wa Hungary
11.


No comments:
Post a Comment