KAA TAYARI KUSHUHUDIA KIVUMBI CHA PEPSI KOMBE LA MEYA 2014.
MASHINDANO ya Pepsi Kombe la Meya Jiji la Mwanza
2014 kuanza kutimua vumbi Agosti 2 mwaka huu na Bingwa kujinyakulia mzigo wa kitita cha
Sh. Milioni sita, wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.
Mwaka huu jumla ya timu 22 zitashiriki ambapo timu 12 zitatoka katika Kata
12 za Jimbo la Nyamagana na timu
nyingine 12 zitatoka katika vikundi na asasi mbalimbali za kijamii zilizopo
jimboni humo.
![]() |
| Balozi wa Habari wa Pepsi Kombe la Meya 2014, Albert G. Sengo akizungumza na wanahabari kuhusiana na taratibu za michuano hiyo zitakavyokuwa. |
Mashindano
haya yanafanyika kwa mwaka wa pili mfululizo chini ya udhamini wa
Kampuni ya SBC inayotengeneza vinywaji baridi kupitia kinywaji chake cha
Pepsi ambapo kwa mwaka huu yameboresha zaidi kwa kuhakikisha vifaa
vitakavyotolewa vinakuwa na ubora ikiwa pia na ongezeko la ukubwa wa
zawadi za washindi. “Lengo
kubwa la mashindano haya ni kuwezesha vikundi vya vijana wajasiriamali,
kuleta umoja, hamasa, kuendeleza vipaji vya soka, mshikamano na
burudani, lakini pia kuviwezesha mitaji ya kuendesha shughuli zao
kupitia mashindano ya soka ili kuvijengea uwezo,”
Zawadi
kwa washindi mwaka huu zimeongezeka ambapo bingwa atajinyakulia Bajaji
ya kisasa ya kubeba mizigo na watu wanne yenye thamani ya milioni 4.5 na
fedha tasilimu milioni 1.5 (jumla milioni sita), mshindi wa pili
milioni 2, mshindi wa tatu milioni 1 huku mfugaji bora, timu yenye
nidhamu na mwamuzi bora kuzawadiwa Sh. Laki mbili.
Awali
meneja wa kamati ya mashindano ya Pepsi Kombe la Meya 2014, Bitegeko
(wa kwanza kulia) alieleza kwamba timu zitakazoshiriki michuano hiyo
zimegawanywa katika makundi manne ambapo kundi A litakuwa na timu sita,
kundi B, C na D kila moja litakuwa na timu tano, mzunguko wa kwanza
utachezwa kwa mtindo wa ligi katika makundi na hatua ya robo fainal timu
zitacheza kwa mtoano hadi kupata timu mbili zitakazo cheza fainali ili
kumpata bingwa kwa mwaka 2014.



No comments:
Post a Comment