Picha Mbalimbali Kutoka Bunge Maalum La Katiba Dodoma

Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiwaeleza
jambo wajumbe wa Bunge maalum la Katiba Edward Lowassa (mwenyeshati
Jeupe) na Philemon Ndesamburo, Ndani ya Ukumbi wa Bunge leo Mjini
Dodoma.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Askofu Mstaafu Donald Mtetemela akiongoza sala ya asubuhi ndani ya ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mufti, Sheikh Thabit Noman Jongo akiongoza dua ya asubuhi ndani ya ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.

Mjumbe wa
Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Mahusiano na Uratibu Steven Wassira akiwaeleza jambo wajumbe wenzie Bi.
Anna Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Richard Ndassa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Sumve, kabla
ya kuingia katika Ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.

Mjumbe wa
Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi John Magufuli
akimweleza jambo Mjumbe mwingine ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo
Bw. John Mnyika Mapema leo Mjini Dodoma.

Wajumbe
wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Ismail Aden Rage (mwenye kanzu) na Hashim
Rungwe wakielekea katika ukumbi wa Bunge mapema leo Mjini Dodoma.Picha na Hassan Silayo
No comments:
Post a Comment