Mh Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu alipo zindua magari yalionunuliwa kwa ajili ya kupambana na Ujangili

Mh
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akitelemka katika moja ya
gari ambalo alilizindua kwa ishara ya kuzindua magari mengine yote
yatakayotumika kupambana na ujangili.

Mh Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akielekea kuongea na wanahabari baada ya uzinduzi huo

Haya ndiyo Magari ambayo yamezinduliwa Rasmi kwa ajili ya kupambana na majangili

Mh Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akizungumza na wanahabari.Picha zote na Maliasili zetu Blog
HII NDIO HOTUBA YAKE KAMILI
Ndugu Wanahabari:
Katika kutekeleza maazimio ya Bunge, na ahadi ya serikali kwa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira, leo nimekamilisha
utaratibu wa kuzitoa silaha zilizokuwa chini ya TRA tangu mwezi wa
Novemba mwaka 2012, ili kuzikabidhi kwa wapiganaji katika Hifadhi za
Taifa, Mamlaka ya Ngorongoro, na Mapori ya Akiba kote nchini kwa lengo
la kupambana na ujangili. Silaha hizi 500 aina ya AK47 ziligharimu
jumla yaSh.427milioni kuzinunua, na leo Wizara yangu inatoa Shs.212
milioni kwa ajili ya kulipia kodi na ushuru mbalimbali ili Mamlaka ya
Mapato Tanzania TRA iziruhusu kutolewa.
No comments:
Post a Comment