HELKOPTA YA CHADEMA YAFANYA KUFURU, YARUSHA VIPEPERUSHI VYA CHADEMA CCM MKOA WA IRINGA
Mambo yanazidi
kuwa matamu katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Iringa
Vijijini, ambapo leo asubuhi helkopta ya Chadema iliuteka mji wa Iringa
kwa kurusha vipeperushi vya mgombea wao Grace Tendega, katika maeneo
mbalimbali ya mji wa Iringa hasa katika stendi kuu ya mabasi na zingine
zilitua Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Iringa.
Kwa
mujibu wa shuhuda ambaye ofisi yake ipo mkabala na Ofisi za CCM,
alisema kuwa majira ya saa nne leo asubuhi waliona helkopta ya Chadema ikipita kwa
chini karibu na majengo huku ikidondosha vipeperushi katika maeneo hayo.
"Mimi
na wenzangu tulishituka na kutoka nje kuiona helkopta hiyo, kwanza
tulidhani inatua lakini haikuwa hivyo. tuliona ikirusha vipeperushi
ambavyo vingine vilitua jengo la CCM, baada ya hapo ikapaa zaidi angani
na kuelekea upande wa kusini mwa Mji wa Iringa," alisema dada huyo.
Chadema ilitangaza kwamba leo inaanza kampeni
katika Jimbo la Kalenga kwa kutumia helkopta maarufu kama Chopa, na
wangeanzia Kijiji cha Wangama alikozaliwa mgombea wao Grace Tendega.

No comments:
Post a Comment