TENDEGA ACHUKUA FOMU ZA UBUNGE JIMBO LA KALENGA
Mgombea
wa Chadema jimbo la Kalenga Grace Tendega akipunga mkono kwa wanachama
wa chama hicho waliompokea katika eneo la Igumbiro Km 8 toka mjini
Iringa
Jeshi
la polisi likiwa tayari limejipanga kuweza kuwazuia wanachama wa
Chadema waliokuwa wametoka kumpokea mgombea wa ubunge jimbo la Kalenga
na askari akiwa mbele ya gari la waandishi akiwazuia kupita (picha zote
na Denis Mlowe)
Baadhi
ya wanachama wa Chadema wakiwa katika foleni ya kumsindikiza mgombea
wao Grace Tendega kuchukua fomu za kugombea jimbo la Kalenga
Jeshi
la polisi likiwa tayari limejipanga kuweza kuwazuia wanachama wa
Chadema waliokuwa wametoka kumpokea mgombea wa ubunge jimbo la Kalenga
na askari akiwa mbele ya gari la waandishi akiwazuia kupita (picha zote
na Denis Mlowe)
Msamamizi
wa Uchaguzi jimbo la Kalenga Pudenciana Kisaka akimkabidhi fomu za
kugombea uchaguzi wa ubunge jimbo la hilo Grace Tendega wa Chadema
katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa jana.
========== ========= =========
TENDEGA ACHUKUA FOMU ZA UBUNGE JIMBO LA KALENGA
Na Denis Mlowe,Iringa.
MGOMBEA
ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(
Chadema), Garce Tendega jana amechukua fomu ya kuwani kiti hicho huku
msafara wake ukikumbana na kizuizi cha Jeshi la Polisi Mkoani hapa
kutokana na kutokuwa na kibali cha kuandamana na kumshikiria diwani wa
kata ya Mivinjeni Frank Nyarusi.
Msafara
huo ulipokelewa maeneo ya Igumbiro kilometa 8 toka Iringa mjini ukiwa
unasindikizwa na pikipiki zaidi ya 50 na magari ya M4C zaidi ya 4 na
gari nyingine ndogondogo 6 na kusababisha msafara huo kusimama zaidi ya
saa moja baada ya jeshi la polisi kuwazuia katika mlima Ipogoro.
Maafisa
wa Polisi waliofika kuzuia masafara huo walisemna wasengeweza kuruhusu
kupita katikati ya mji kwa madai hayo ni maandamani batili na
kusababisha ubishani kati ya uongozi wa jeshi hilo na waratibu wa
mapokezi ya mgombea huyo.
Akizngumza
mara baada ya kuchukua fomu, Grace Tendega alisema moja ya changamoto
ambayo inampa nafasi ya kushinda uchaguzi huo mdogo ni wapinzani kujenga
woga hadi kufikia hatua ya kutumia jeshi la polisi kuwazuia kwenda
kuchukua fomu za kugombea.
“ Huu
ni mwanzo tu wa mapambano ya kulikomboa jimbo la Kalenga kutoka kwa
chama tawala ambacho kwa miaka zaidi ya Hamsini maisha ya wananchi
wamebaki kuwa na maisha yale yale ni zamu yetu sasa kuwakomboa
wanakalenga na Tanzania kwa jumla hivyo wananchi wakinipa ridhaa hakika
nitawaletea maendeleo kwa kushirikiana nao” alisema Tendega.
Mgombea
huyo alisema Chadema kimejiandaa kushinda na kilichotokea katika
msafara wake ni mwanzo tu wa mapambano hivyo chama kiko tayari kwa
mapambano ya kuwapata wapiga kura wataoweza kuwaondoa madarakani .
Tendega
aliwataka wakazi wa Jimbo la Kalenga kutokuwa na hofu kutokana na
matukio yanayoweza kujitokeza kama lilivyotokea la kuzuiliwa na jeshi la
polisi ila wajitokeza kwa wingi kuunga mkono harakati hizo za
ukombozi.
Alisema
wananchi wa jimbo la Kalenga wanatakiwa wachague kiongozi atakayewafaa
na si kuwatesa na kuwatumiakia na sio kuwatawala katika kuwaletea
maendeleo ya jimbo la Kalenga.
Mgombea
huyo alifanikiwa kuondoka maeneo hayo baada ya jeshi la polisi
kumruhusu kuondoka maeneo hayo bila msafara wa magari na pikipiki hizo
hadi katika ofisi zaMsimamizi wa uchaguzi Pudenciana Kisaka ambaye pia
ni Mkurugenzi wa Jimbo la Iringa Vijijini na kukabidhiwa nyaraza
mbalimbali za tume ya taifa ya uchaguzi zikiwamo sheria kanuni na katiba
ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uchaguzi
huo unafanyika kufuatia kufariki kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la
Kalenga na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa na mgombea wa Chadema
atapambana na mtoto wa marehemu Dk Mgimwa anayejulikna kwa jina la
Godfrye Mgimwa.
No comments:
Post a Comment