Header Ads

Soma Msimamo wa Mbunge wa Arumeru Mashariki-Chadema na mjumbe wa bunge maalum la katiba Joshua Nassari Juu ya Sakata la Posho Bunge la Katiba


Mbunge wa Arumeru Masharikina mjumbe wa bunge maalum la katiba Joshua Nassari
--
 Nimeona nukuu kwenye gazeti la nipashe la leo. Kumsingi ike nujuu si ya kwangu ni 

nineshazungumza na Mhariri wa jipashe Bw. Kwayu.Sijui kama nukuu ile imewekwa kwa 

kukosea au kwa makusudi, wameahidi kurekebisha makosa lakini ni vyema jikaweka 

msimamo wangu hapa.

Kwa hali halisi ya maisha ya kawaida ya Mtanzania wa shilingi laki 3 ni fedha nyingi. Na 

taasisi ya Bunge ndiyo inayopaswa kuwqpigania hawa watanzania ili vipato vyao vipande 

lakini taasisi hii siku zote imekubali kuwa upande wa serikali badala ya kuisimamia serikali 

kwa niaba ya wananchi.


Fedha hiyo bado ni nyingi mno kama kipato cha mtanzania kinabaki kuwa hapo kilipo.
 
Kabla ya kupigania ongezeko ambalo linaweza wakati mwingine likawa na mantiki, ni vyema 

wabunge wakaifanya kwanza kazi yao ya kupigania maisha bora na maslahi bora kwa 

wananchi hiki hiyo mantiki yao iweze kuonekana. Itherwise na sisi wabunge tutakuwa ni 

sehemu ya hali ngumu ya maisha ya watanzania ambao bado wanajifungulia sakafuni na 

hawana maji safi ya kunywa. 
Na

Joshua Nassari (MB) na mjumbe wa bunge maalum la katiba.

No comments:

Powered by Blogger.