SOMA BARUA YA WAZIKUTOKA KWA MBUNGE WA KILWA KASKAZINI-CCM MURTAZA MANGUNGU KUHUSU SUALA LA URAIA PACHA(DUAL CITIZENSHIP)

MHE. Murtaza Mangungu(MB)Kilwa Kaskazini akiwa na Bwana Phanuel Ligate (Mwakilishi wa Diaspora) Kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma November 2012
--
Habari
za Wakati huu ! Nimekuwa nikifuatilia mijadala na maoni mbalimbali
kupitia mitandao na wengine walionitumia e-mail au kunipigia simu. Kwa
Kuwa mawasiliano yetu hayakuwa bayana nilidhani nitoe ufanunuzi kuhusu
suala la uraia pacha (Dual citizenship ) . Awali ya yote Naomba radhi
sana ikiwa maelezo ninayotoa nitamkwaza yeyote ila naomba iaminike si
kusudio langu, pengine ni uelewa na nitakuwa tayari kukosolewa
Nawapongeza sana kwa jitihada kubwa mnazozifanya ili kufikia lengo , nawahakikishia Kuwa nitakua wa mwisho kukubaliana na suala hili kutoingizwa kwenye katiba mpya. Binafsi naelewa kila neno mnalomaanisha na faida ya kuwapo kwa 'dual citizenship " kwa faida ya nchi yetu na ustawi maridhawa wa jamii zetu kwa ujumla.
Ukisoma katiba yetu ya sasa na rasimu ya katiba mpya hakuna kipengele ambacho kinazungumza Aina ya uraia na pia hakuna tafsiri ya Raia ni ipi . Ibara ya ya katiba ya Mwaka 1977 kifungu 13(1)(3) ,17(1), 22(2), 28(1), 29(1)(2)(3) zimetamka Raia bila kutafsiri 'Raia" ni nani , Aidha kwenye vifungu au kwenye jedwali la tafsiri www.katiba.go. tz Rasimu ya katiba ya 2013 Ibara ya 38 imetamka ya uraia bila ya kutoa
kwa ufafanuzi 'Raia " ni nani au aina za uraia. Ukisoma sheria ya uraia
ya Mwaka 1995( The Tanzania Citizenship Act, 6 of 1995 )http://polis.parliament.go. tz/PAMS/docs/6-1995.pdf ndipo
unapata tafsiri zote kuwa raia wa Tanzania ni nani na aina zipi za
uraia kwa mujibu wa sheria. Kimsingi aina za uraia ama 'Dual Citizenship
" si suala la kikatiba bali ni sheria ya Uraia . Zipo jitihada kubwa za
kiushawishi kutoka kwa Mh. Rais Dr. Kikwete , Mh. Membe pamoja na
viongozi wa Sekretarieti ya CCM (Mh. Madelu Mwigulu Mchemba na Ndugu
Nape Nnauye) Kuwa lazima suala hili lipewe kipaumbele na msimamo wa
chama 'CCM" ni Kuwa lazima pawepo na haki hii ya uraia pacha.
Zipo namna mbili za kuwasilisha hili kwenye Bunge la katiba
I. Kupeleka jedwali la mabadiliko ( schedule of amendment )
II. Kupeleka mabadiliko ya kifungu kwenye Kamati ili iwasilishwe bungeni kwa mjadala
Binafsi nimeamua kutumia njia zote ili kuhakikisha hakuna mkwamo. Nawashukuru sana wale wote walioniagiza nihakikishe suala hili nalisimamia ipasavyo , Ndugu Iddy Sandaly, Alhaj Kalala , Ndugu Phanuel Ligate , Richard Mwandemani ,Khalfani Lyimo na wengineo wengi. Ninawahakikishia Kuwa nitalisimamia jambo hili kwa kadiri ambavyo Mungu ataniwezesha. Siwezi kusahau hata kidogo maisha ya wema niliyoishi na wenzangu huko ughaibuni , pia hakuna namna itakayonifanya nisahau umuhimu wa jambo hili ikiwa binafsi ni miongoni mwa ' wahanga'' wa janga hili
Ahsanteni
Murtaza Mangungu(MB)
Kilwa Kaskazini
Nawapongeza sana kwa jitihada kubwa mnazozifanya ili kufikia lengo , nawahakikishia Kuwa nitakua wa mwisho kukubaliana na suala hili kutoingizwa kwenye katiba mpya. Binafsi naelewa kila neno mnalomaanisha na faida ya kuwapo kwa 'dual citizenship " kwa faida ya nchi yetu na ustawi maridhawa wa jamii zetu kwa ujumla.
Ukisoma katiba yetu ya sasa na rasimu ya katiba mpya hakuna kipengele ambacho kinazungumza Aina ya uraia na pia hakuna tafsiri ya Raia ni ipi . Ibara ya ya katiba ya Mwaka 1977 kifungu 13(1)(3) ,17(1), 22(2), 28(1), 29(1)(2)(3) zimetamka Raia bila kutafsiri 'Raia" ni nani , Aidha kwenye vifungu au kwenye jedwali la tafsiri www.katiba.go.
Zipo namna mbili za kuwasilisha hili kwenye Bunge la katiba
I. Kupeleka jedwali la mabadiliko ( schedule of amendment )
II. Kupeleka mabadiliko ya kifungu kwenye Kamati ili iwasilishwe bungeni kwa mjadala
Binafsi nimeamua kutumia njia zote ili kuhakikisha hakuna mkwamo. Nawashukuru sana wale wote walioniagiza nihakikishe suala hili nalisimamia ipasavyo , Ndugu Iddy Sandaly, Alhaj Kalala , Ndugu Phanuel Ligate , Richard Mwandemani ,Khalfani Lyimo na wengineo wengi. Ninawahakikishia Kuwa nitalisimamia jambo hili kwa kadiri ambavyo Mungu ataniwezesha. Siwezi kusahau hata kidogo maisha ya wema niliyoishi na wenzangu huko ughaibuni , pia hakuna namna itakayonifanya nisahau umuhimu wa jambo hili ikiwa binafsi ni miongoni mwa ' wahanga'' wa janga hili
Ahsanteni
Murtaza Mangungu(MB)
Kilwa Kaskazini
No comments:
Post a Comment