 |
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Robin Goetzche (kushoto)
akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Dola za Kimarekani 64,000,
Mwasisi na Mkurugenzi wa Taasisi ya ACE Africa, Joanna Waddington katika
hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TBL, Dar es Salaam jana. Msaada huo
uliotolewa na TBL kwa niaba ya Kampuni ya Sabmiller Afrika ni kwa ajili
ya kusaidia kuboresha ufugaji wa mbuzi, kuongeza uzalishaji wa mazao ya
vyakula na sekta ya maji katika Wilaya ya Arumeru, mkoani
Arusha.Anayeshudia makabidhiano hayo ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria
wa TBL, Steve Kilindo.
 |
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo akielezea mikakati ya TBL ya kusaidia jamii hasa katika sekta ya maji.
 |
| Robin akielezea sababu ziliifanya SABMiller/TBL kuisaidia taasisi ya ACE Africa. |
Mwasisi
na Mkurugenzi wa Taasisi ya ACE Africa, Joanna Waddington akitoa
shukurani kwa SABMiller/TBL kupatiwa msaada huo muhimu kuboresha maisha
ya jamii Arumeru. (PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
No comments:
Post a Comment