Picha:Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha Ashiriki Maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Lizzy Lloyd akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China
nchini Tanzania, Mhe. Lv Youqing akitoa neno la shukrani kwa Benki ya
Standard Chartered kwa kuandaa hafla hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akizungumza
kwenye halfa ya kuadhimisha mwaka mpya wa China, iliyoandaliwa na Benki
ya Standard Chartered na kufanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency
Kilimanjaro, Dar es Salaam. Wakati wa hafla hiyo Balozi Gamaha
aliupongeza Ubalozi wa China katika kusaidia na kuchangia maendeleo ya
Tanzania. Pia Balozi Gamaha aliipongeza Benki ya Standard Chartered kwa
kushirikiana na Ubalozi wa China nchini katika kurahisisha biashara
kati ya Tanzania na China.
Wageni waalikwa walioshiriki hafla hiyo.
Balozi Gamaha akizungumza na Waandishi wa Habari.
Balozi Gamaha (kulia) akimsikiliza
Bw. Nathaniel Kaaya, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Asia na
Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
wakati wa hafla hiyo. Wengine wanaosikiliza kutoka kushoto ni Bw. Iman
Njalikai na Bw. Emmanuel Luangisa, Maafisa Mambo ya Nje.Picha na Reginald Kisaka
No comments:
Post a Comment