PICHA KUTOKA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA NCHINI: KAMISHNA WA MAGEREZA NCHINI ZAMBIA AITIMISHA ZIARA YAKE NCHINI TANZANIA
Baadhi ya Wasanii machachari wa Kikundi cha Sanaa za ngoma cha Chuo
cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Dar es salaam kikitumbuiza mbele ya
Mgeni Rasmi
pamoja na wageni mbalimbali katika hafla ya kumuaga Kamishna wa
Magereza Zambia Percy Chato iliyofanyika katika Bustani ya Bwalo la
Maafisa la Ukonga.
Kikundi cha Sanaa za ngoma cha Chuo cha Maafisa wa Magereza
Ukonga, Dar es salaam kikitumbuiza mbele ya Mgeni Rasmi pamoja na wageni
mbalimbali katika hafla ya kumuaga Kamishna wa Magereza Zambia Percy
Chato iliyofanyika katika Bustani ya Bwalo la Maafisa la Ukonga.
Kamishna wa Magereza wa nchini Zambia Percy K. Chato (mwenye
suti) akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa Ofisi ya Magereza Mkoa wa
Kilimanjaro, Gereza Karanga na Kiwanda cha Viatu Moshi alipotembelea
kiwandani hapo mapema juma hili. Nyuma yake ( wa kwanza kushoto) ni
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt. Juma Ali
Malewa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi
Mwandamizi Hamis Nkubasi, Mkaguzi Msaidiz wa Magereza Geofrey Mpagike
kutoka Makao Makuu ya Magereza na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Magereza Zambia John Yumbe (aliyegeuka nyuma) ambaye pia ni Mkurugenzi
wa Miradi Makao Makuu ya Magereza Zambia.
Kamishna Jenerali wa Magereza Tanzania John C.Minja pamoja na Kamishna
wa Magereza wa Zambia Percy K.Chato wakiingia katika viwanja vya Bustani
ya Bwalo Kuu la Maafisa Ukonga, Dar es salaam katika tafrija fupi ya
kumuaga Kamishna wa Magereza wa Zambia baada ya kumaliza
ziara ya siku sita nchini Februari 13,2014.
Kamishna wa Magereza nchini Zambia Percy K. Chato (kushoto)
akikabidha zawadi kwa Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja
(katikati) kutoka kwa uongozi wa Magereza nchini Zambia.
Kamishna Jenerali wa Magereza
John Minja (kushoto) akikabidhi zawadi maalum iliyoandaliwa na uongozi
wa magereza kwa Kamishna wa Magereza wa Zambia Percy Chato (katikati)
Kamishna
wa Magereza wa Zambia Percy K. Chato akishiriki mlo wa jioni katika
hafla ya kumuaga iliyoandaliwa na mwenyeji wake Kamishna Jenerali wa
Magereza Tanzania John C. Minja, Februari 13,2014
Kamishna wa Magereza wa nchini Zambia Percy K. Chato (mwenye suti)
akiwa katika sehemu ya mwisho baada ya viatu kukamilika na tayari kwenda
sokoni.Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza
nchini Dkt Juma Ali Malewa akitoa maelezo kwa Kamishna Percy juu ya
viatu vinavyotengenezwa kiwandani hapo.
Kamishna wa Magereza wa nchini Zambia Percy K. Chato (mwenye suti)
akiangalia bidhaa katika moja ya duka
linaloyouza bidhaa zisizo na tozo ya kodi (Duty Free Shops) kwa
watumishi wa Jeshi la Magereza Mkoani Kilimanjaro, mwenye shati la draft
ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Nchini Dkt Juma Ali
Malewa aliyeambatana na Kamishna wa Zambia katika ziara hiyo.Kulia ni
afisa msimamizi wa duka hilo.
Mkuu wa Kiwanda cha viatu Karanga Moshi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa Magereza Venant Kayombo (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo kwa
Kamishna wa Magereza wa nchini Zambia Percy K. Chato (mwenye suti) hatua
za awali za utengenezaji wa viatu kiwandani hapo.
Kamishna wa Magereza wa Zambia Percy K. Chato akitoa neno la
shukrani na kuwaaga maafisa na watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania
(hawapo pichani) katika hafla fupi iliyoandaliwa maalum kwa ajili yake
katika Bustani ya Bwalo Kuu
Ukonga, Dar es salaam, Februari 13,2014
Kamishna
Jenerali wa Magereza Tanzania akisakata rumba pamoja na Kamishna wa
Magereza nchini Zambia Percy K. Chato (kuli).Picha zote Insp. Deodatus
Kazinja, wa Jeshi la Magereza
No comments:
Post a Comment