ASIA IDAROUS AWASHUKURU WADAU
..Kwa kusapoti miaka 10 ya ‘Lady in red’
.. kuwa jukwaa la kimataifa
Na Andrew Chale
MAMA
wa Mitindo nchini na Mkurugenzi wa Fabak Fashins, Asia Idarous Khamsin
amewashukuru wadau mbali mbali kwa kuendelea kulinga mkono onyesho la
Mitindo la kila mwaka la 'Lady in red' ambalo kwa mwaka huu limeweza
kutimiza miaka 10, tokea kuanzishwa kwake huku likiwa la mafanikio kwa
kuibua wanamitindo wakubwa hapa nchini.
Akizungumza
Dar es salaam, katika ofisi za Fabak zilizopo Msasani jirani na Kwa
Mwalimu Nyerere, Asia Idarous alishukuru wadau mbali mbali waliojitokeza
siku hiyo sambamba na wadhamini waliofanikisha kwa shughuli hiyo kubwa
hapa nchini.
Asia
alisema ni jambo la fadhira kwa kushukuru huku akiahidi kuboresha kama
kulikuwa na mapungufu ya hapa na pale. "Muungwana ni vitendo, ‘Lady in
red Super brand, 10th Anniversary’ ilikuwa ni ya kipekee kwa mwaka huu,
hivyo nawashukuru nyote kwa kuliunga mkono jukwaa la Lady in red 2014,
kwa kutimiza miaka hii 10" alisema Asia Idarous.
Na
kuongeza kuwa, kuelekea onyesho la mwakani kwa mwaka 2015, jukwaa hilo
la Lady in Red, linatarajia kuwa la kimataifa ikiwemo wabunifu wa
kimataifa kuonyesha ubunifu wao hapa nchini.
"Kwa
sasa tunaelekea anga za kimataifa kupitia jukwaa hili hili la Lady in
red, zaidi ni kuendelea kuliunga mkono ilikutimiza ndoto hizi, na hii
itasaidia kufungua milango ya wabunifu wetu kujiuza nje ya mipaka yetu"
alisema Asia Idarous.
Onyesho
hilo la Lady in red 2014, lililotimiza miaka 10, lilifanyika Februari
14, ndani ya ukumbi wa kisasa wa ndani ya hoteli yenye hadhi ya nyota
tano ya Serena, ambapo siku hiyo pia ilikuwa ni maalumu kwa wapendanao
duniani 'Valentine Day' watu wa kada tofauti wakiwemo mastaa na watu
maarufu walijumuika kwa pamoja kuliunga mkono onyesho hilo.
Wabunifu
mbali mbali wakiwemo magwiji na chipukizi walipata kuonyesha mitindo ya
ubunifu kwenye jukwaa hilo na kuvutia wengi siku hiyo. mbali na
ubunifu wa mavazi, pia liliendana sambamba na mapambano dhidi ya dawa za
kulevya, huku asilimia kadhaa za mapato yake yalipelekwa kusaidia
waathirika wa dawa za kulevya.
Kwa
upande wa burudani, wapendanao na wadau waliojitokeza walishuhudia
burudani safi kutoka kwa wasanii mkali wa nyimbo za asili, Wanne Star
na mkali wa R&B na Afro pop, Nemo ambaye hadi sasa anatamba na
vibao mbali mbali ikiwemo My Number One, alichomshirikisha Omy Dimpoz.
Pia
Asia Idarous aliwashukuru wadhamini wakuu, ikiwemo kinywaji cha Zanzi na
Rasta za Darling. Wengine ambao wamekuwa chachu ya mafanikio ya jukwaa
hilo ni pamoja na Michuzi Blog, Vijimambo blog, Dj Bula, CXC, Times fm,
Clouds media, michuzi media group, channel ten, Elite Computer,
Eventlites, One touch-solution, Raysa Style, Paka Wear, Magic fm, DTV,
Jambo Leo, I View media, Vayle Spring, Voice of American na wengine
wengi.
Mwisho
Habari na Andrew Chale, Picha zote crediti kwa Michuzi blog.
No comments:
Post a Comment