WENYEVITI WA CCM KATA ZOTE WILAYA YA KINONDONI 'WAJIFUNZA' KILIMO CHA ZABIBU DODOMA
Meneja
wa Shamba la zao la zabibu lililopo Chnangali, Wilaya ya Chamwino
mkoani Dodoma, Ronaldaka akisoma taarifa ya shamba hilo, Washiriki wa
semina ya Wenyeviti wa CCM kutoka kata za wilaya ya Kinondoni, mjini Dar
es Salaam, walipotembelea shamba hilo, jana kujua zao za zabibu
linavyozalishwa, changamoto na faida za kilimo cha zao hilo.
Meneja
wa shamba akiwaonyesha mfumo wa maji unavyofanya kazi kuyavuta kutoka
visimani kabla ya kumwagiliwa shambani. Wasita kushoto ni kiongozi wa
msafara huo, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni, Mzee Madenge
Wajumbe wakionyeshana kitu wakati wakitazama bwawa maalum la maji ya kumwagilia mashamba ya zabibu
Meneja huyo akiwaonyesha wajumbe maji yanavyoingia kwenye vishina vya miti ya zabibu
Mwenyekiti
wa zamani wa klabu ya Simba Hassan Dalali (watatu kushoto) ambaye ni
mjumbe wa semina hiyo, akiwaeleza jambo wenzake kwenye shamba la zabibu
Meneja
wa shamba akimpa maelezo mkuu wa msafara mzee Madenge. Kulia aliyevaa
kijani ni Katibu wa CCM, wilaya ya Dodoma mjini Saad Kusilawe. Wenyeviti
wa CCM katika kata 31 za wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, wapo
mkoani Dodoma kwenye semina au mafunzo ya siku nne kwa ajili ya kujinoa
zaidi weledi wao katika masuala mbalimbali ya kijamii na uongozi. Imetayarishwa na theNkoromo Blog






No comments:
Post a Comment