Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan na kumlipa fidia ya gharama alizotumia katika shauri la madai ya kutotendewa haki na gazeti hilo, baada ya kuandika habari ambazo zilizomuhusisha mbunge huyo na biashara ya dawa za kulevya bila kumpa nafasi ya kujieleza.

Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan akieleza malalamiko yake mbele ya
Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari (MCT), kuhusiana na madai ya
kukashifiwa na gazeti la Raia Mwema na Mwanahabari kwa kumhusisha na
biashara ya dawa za kulevya, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni
Mhariri wa Gazeti la Raia Mwema, Godfrey Dilunga. Picha na Joseph
Zablon.
---
Gazeti la Raia Mwema limetakiwa kumwomba radhi ndani ya wiki
mbili,Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan na kumlipa fidia ya gharama
alizotumia katika shauri la madai ya kutotendewa haki na gazeti hilo,
baada ya kuandika habari ambazo zilizomuhusisha mbunge huyo na biashara
ya dawa za kulevya bila kumpa nafasi ya kujieleza.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao
cha Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari (MCT),kilichofanyika makao
makuu ya baraza hilo jana, Mwenyekiti wa MCT, Jaji Thomas Mihayo
alisema, baada ya kamati hiyo kusikiliza pande zote mbili imebainika
kuwapo kwa upungufu wa kitaaluma katika habari hiyo.
Gazeti la Raia Mwema katika toleo namba 309 la
Julai 31, mwaka huu kulikuwa na habari ambayo kichwa chake cha habari
kilisomeka ‘Idd Azzan Mbunge au muuza madawa ya kulevya’ na ndani ya
habari hiyo kulikuwa na tuhuma kuwa anajihusisha na biashara ya dawa
hizo huku baadhi ya vifungu vikimkariri mbunge huyo.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea.........
No comments:
Post a Comment