DK MVUNGI ALAZWA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI BAADA YA KUJERUHIWA VIBAYA

Dkt. Sengondo Mvungi, akiwa kwenye gari
la kubeba wagonjwa, baada ya kufikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH), akihamishiwa hapo kiutoka Hospitali ya Tumbi, Kibaha Jumapili
Novemba 3, 2013.

Dkt. Sengondo Mvungi, amejeruhiwa vibaya
sehemu za kichwani na usoni, baada ya kukatwa mapanga, nyumbani kwake,
Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya jiji, majira ya saa sita usiku Jumamosi
Novemba 2, 2013.
Kwa mujibu wa taarifa za ndugu na polisi,
Dkt. Mvungi ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi wa Sheria, Chuo Kikuu cha
Bagamoyo, mkoani Pwani, alicharangwa mapanga, baada ya kutaka kujua
nini kilichokuwa kikiendelea kufuatia mabishano baina ya mkewe na watu
hao ambao walitishia kumuua endapo asingewapa fedha.
Taarifa zinasema, watu hao sita wengine
wakiwa nje ya nyumba kwa nia ya kujihami endapo wangevamiwa na majirani,
walivamia nyumba hiyo yenye ghorofa moja, na kumkuta mkewe Dkt. Mvungi
wakati huo Dkt. Mvungi akiwa kwenye chumba tofauti katika nyumba hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, wavamizi
walipoona mke wa Dkt. Mvungi anachelewa kutekeleza maagizo yao,
walifyatua baruti na hapo Dkt. Mvungi akajaribu kuelekea kulikotokea
mlio huo na ndipo alipokutana na mapanga ya kichwani na usoni.
Uchunguzi wa awali wa polisi umeonyesha
kuwa tukio hilo ni la kihalifu, kwani watu hao ambao kwa sasa wanatajwa
kama majambazi, waliiba fedha, simu na laptop, hali inayoonyesha wazi
kuwa nia yao ilikuwa ni kutekeleza wizi.
Dk. Mvungi aliwahi kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi.
No comments:
Post a Comment