Header Ads

WAKAZI WA JIJI LA DAR WAJITOKEZA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS MUDA HUU KWA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MWILI WA JULIUS NYAISANGA

 Msafara wa Magari ambao moja wapo (la mbele) likiwa limebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Julius Nyaisanga ukiingia kwenye viwanja vya leaders muda huu kwaajili ya wakazi wa jiji la Dar kuweza kutoa heshima zao za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga kabla ya Kusafirisha Kwao Tarime Mkoani Mara


Baadhi ya Ndugu, Jamaa na marafiki wakibeba jeneza lenye Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga Kwaajili ya kupeleka sehemu husika tayari kwa kutoa heshima za mwisho kwa wakazi wa jiji la Dar waliofika katika viwanja vya leaders muda huu

Sehemu Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga litakapowekwa kwaajili ya wakazi wa jiji la dar kuweza kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Tarime Mkoani Mara
 Baadhi ya wakazi wa jiji la dar waliojitokeza katika viwanja vya leaders muda huu
Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar wakisubiria Kutoa Heshima zao za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga Kabla haujasafirishwa kupelekwa Kwao Tarime Mkoani Mara.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza blog

No comments:

Powered by Blogger.