Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri. Neville Meena akizungumza
mara baada ya waandishi wa habari kumaliza maadamano yao ya Amani kutoa
ujumbe wao kwa jeshi la Polisi kutokana na kupot
eza maisha kwa
mwandishi wa habari Marehemu Daudi Mwangosi aliyeuwawa katika vurugu
kati ya Polisi na Wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
katika kijiji cha Nyololo Mkoani Iringa hivi karibuni.
IRINGA. KATIBU Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga, amesema sekta ya habari kwa sasa ipo katika wakati mgumu na hatari kuliko wakati mwingine wowote huko.
IRINGA. KATIBU Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga, amesema sekta ya habari kwa sasa ipo katika wakati mgumu na hatari kuliko wakati mwingine wowote huko.
Akizungumza katika uzinduzi wa mkutano wa Jukwaa
la Wahariri Tanzania (TEF) mjini Iringa jana, alisema hatari hiyo
inatokana na kutokuwepo kwa sheria bora za kusimamia usalama wa
waandishi wa habari na watoa habari nchini.
Alisema pamoja na hali hiyo inayoibua mapambano
baina ya wadau wa tasnia hiyo na Serikali wahariri na waandishi wa
habari wana jukumu la kusimamia ukweli katika kutekeleza majukumu yao na
kufanya kazi kwa weledi.
“Tasnia ya habari kwa sasa ipo katika kipindi
kigumu na waandishi wapo katika hatari kuliko wakati mwingine wowote,
njia pekee kujilinda na hali hiyo ni waandishi na wahariri kuandika
habari za kweli na kutekeleza majukumu yao kwa weledi na
uadilifu,”alisema Mukajanga.
Mukajanga aliwataka wahariri kuepuka kuingia
kwenye mgawanyiko wa kutumikia makundi ya watu ama watu binasfi kwa
maelezo kuwa kufanya hivyo na kujiingiza katika hatari zaidi.
“Epukeni kutumikia makundi ya watu fulani ama mtu binafsi, fanyeni kazi kwa kuzingatia weledi na maadili ya kazi zenu. ”alisema.
Alisema wahariri wanapaswa kuzingatia usalama wa
waandishi wa vyombo vyao kwa kuzingatia na kuangalia uzuri na ubora wa
habari wanazopokea. MWANANCHI
No comments:
Post a Comment