Mwasisi wa Chadema Edwin Mtei (mwenye kofia) akizungumza kwenye mkutano
wa siku tatu wa Baraza la Kanda ya Kaskazini ya chama hicho jijini
Arusha juzi. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Kanda Mchungaji Israel
Natse, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Katibu wa Kanda, Amani
Golugwa. PICHA /FILBERT RWEYEMAMU
ARUSHA. MKUTANO wa Baraza la Uongozi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kask azini juzi uligeuka ukumbi wa ngumi, baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba kushushiwa kipigo.
ARUSHA. MKUTANO wa Baraza la Uongozi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kask azini juzi uligeuka ukumbi wa ngumi, baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba kushushiwa kipigo.
Mwigamba alishushiwa kipigo hicho na baadhi ya
viongozi wenzake wa chama kwa madai ya usaliti na tayari amesimamishwa
uongozi kwa muda usiojulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas
jana alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na viongozi hao wa Chadema
kufikishana polisi.
Alikutwa na zahama hiyo mbele ya viongozi wakuu
wa Chadema Taifa, Mwenyekiti, Freeman Mbowe na mwasisi wa chama hicho,
Edwin Mtei katika Hoteli ya Coridal Spring.
Viongozi hao wamekuwa wakifanya ziara za aina hiyo
nchi nzima, kuimarisha chama na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa
Serikali za Mitaa mwakani na uchaguzi mkuu ujao wa Rais na wabunge mwaka
2015.
Habari kutoka ndani ya mkutano huo zinaeleza kuwa
hatua hiyo ilifuatia tuhuma kwamba Mwigamba alituma ujumbe kwenye
mtandao wa kijamii wa Jamii Forums, unaodaiwa kukichafua chama hicho.
Tukio hilo la aina yake lilitokea wakati viongozi
wote wa juu wa chama hicho, wakiongozwa na Mbowe walipokuwa wakijadili
mustakabali wa chama hicho, mkutano ambao ulihudhuriwa na wabunge karibu
wote wa Chadema wa kanda hiyo.
Hata hivyo, wakati mijadala ikiendelea baadhi ya
viongozi wa chama hicho, akiwamo Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,
Godbless Lema walimtuhumu Mwigamba kutuma ujumbe kwenye mtandao huo,
uliokuwa ukizungumzia ufisadi ndani ya chama hicho, wakidai alitaka
Mwenyekiti Mbowe kukubali kuchunguzwa.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Mwigamba
alisema kuwa baada ya Lema kutoa tuhuma hizo aliungwa mkono na viongozi
wengine na vijana waliokuwa wameimarisha ulinzi, kumvamia na kuanza
kumpiga pamoja na kumnyang’anya kwa nguvu kompyuta mpakato (Laptop),
aliyokuwa nayo, kisha kumpeleka Kituo Kikuu cha Polisi, mjini Arusha.
“Wamenipiga sana na kuniweka ndani, ila nashukuru
Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Arusha (OCCID), alikuja na kunitoa saa
5:00 asubuhi,” alisema Mwigamba.
Alisema kuwa leo katika mkutano wake na waandishi
wa habari ataeleza yote yaliyotokea na hatua atakazochukua, kwa kuwa
yeye ni kiongozi wa juu wa chama.
Hata hivyo, alieleza kwamba bado anashauriana na wanasheria wake kuona kama anaweza kuwachukulia hatua waliompinga. MWANANCHI
No comments:
Post a Comment