Serikali na Kituo cha Demokrasia wakutana.
Baadhi
ya Wawakilishi wa Serikali wakiwa katika kikao cha Kujadili Mapendekezo ya
Vyama vya Siasa juu ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya katiba yaliyowasilishwa
Serikalini tarehe 21 Oktoba 2013, (kutoka kushoto), Naibu Waziri wa Sheria na
Katiba, Bi. Angela Kairuki, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Frederick Werema
na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge ), Mhe. William
Lukuvi (Mb), kikao hicho kimefanyika leo
Katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Wawakilishi wa vyama vyenye wawakilishi Bungeni wakiwa katika kikao
cha Kujadili Mapendekezo ya Vyama vya Siasa juu ya Marekebisho ya Sheria ya
Mabadiliko ya katiba yaliyowasilishwa Serikalini tarehe 21 Oktoba 2013, kikao
hicho kimefanyika leo Katika Ukumbi wa
Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini
Dar es Salaam.
Wajumbe
kutoka Serikalini (kushoto) na Wajumbe kutoka Wawakilishi wa vyama vyenye wawakilishi
Bungeni (Kulia)
wakiwa katika kikao cha Kujadili Mapendekezo
ya Vyama vya Siasa juu ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya katiba yaliyowasilishwa
Serikalini tarehe 21 Oktoba 2013, kikao hicho kimefanyika leo Katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya
Waziri Mkuu Jijini Dar es Salaam.
======== ====== =======
Serikali na Kituo
cha Demokrasia wakutana kujadili Marekebisho ya Sheria
ya Mabadiliko ya katiba.
Na.
Mwandishi Maalum.
Serikali imekutana na Kituo cha Demokrasia nchini ambacho
wanachama wake ni vyama vyenye wawakilishi Bungeni ili Kujadili Mapendekezo ya Vyama vya Siasa
juu ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya katiba ambayo vyama hivyo
viliyawasilisha Serikalini tarehe 21 Oktoba 2013.
Akiongea wakati wa kikao hicho leo Katika
Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu
Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu na Bunge ), Mhe. William Lukuvi (Mb) alifafanua kuwa lengo la kikao
hicho ni kujadili na kuchambua Mapendekezo ya Vyama vya Siasa juu ya
Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya katiba ambayo waliombwa wayawasilishe
rasmi.
“Kikao hiki
kinafanyika kufuatia kikao alichofanya Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete tarehe 15 Oktoba Ikulu Jijini Dar es Salaam na Viongozi wa Vyama
vyenye wawakilishi Bungeni na kuwaomba wawasilishe rasmi maoni yao Serikalini
na sasa kamati ya kitaalam ya Serikali tumekutana nao kujadili na kuchambua
Mapendekezo yao” alisema Lukuvi.
Vyama vya Siasa vilivyo shiriki katika kikao hicho ni; CCM,
CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi, UDP na TLP, kwa upande wa Serikali iliwakilishwa na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu na Bunge), Waziri wa Sheria na Katiba, Naibu Waziri wa Sheria na
Katiba, Msaidizi wa Sheria wa Rais, Msaidizi wa Sheria wa Waziri Mkuu na
Mkurugenzi wa Idara ya Siasa na Bunge
Ofisi ya Waziri Mkuu.
No comments:
Post a Comment