Matokeo ya Nani Mtani Jembe kuanza kutangazwa leo
Mwenyekiti
wa Simba SC, Aden Rage akishangilia na wafanyakazi wa kiwanda cha TBL
Mbeya wanaoshabikia Simba baada ya kuibuka washindi katika shindano la
kuvuta kamba katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa
wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akitambulisha
kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa TBL Mbeya mwishoni mwa
wiki.
Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji Yanga, Mohammed Bhinda akimkabidhi Nancy
Tibanyenda zawadi baada ya timu yake kushinda mchezo wa kuvuta kamba
katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa
kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya.
Wafanyakazi
akinamama wa TBL Mbeya wakishindana kuvuta kamba katika hafla ya
kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho
mwishoni mwa wiki jijini Mbeya.

No comments:
Post a Comment