MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU YAMUACHIA HURU ALIYEKUWA WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAISI ARCADO NTAGAZWA KWA KUTOKUTWA NA HATIA
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imewaachia huru Waziri wa
zamani, Arcado Ntagazwa na wenzake waliokuwa na kesi na kujipatia mali
kwa njia ya udanganyifu zenye thamani ya sh milioni 74.9, baada ya
kuwaona hawana hatia na hawakutenda kosa hilo.
Sambamba
na hilo, mahakama hiyo imemshauri mlalamikaji katika kesi hiyo ambaye
ni Noel Severe kufungua kesi ya madai kama walivyofanya hivi karibuni,
ambapo walifungua kesi ya madai dhidi ya Ntagazwa.
Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Gene Dudu, alisema kuwa kesi hiyo ya
jinai namba 108/2012 aliyoitolea hukumu jana, haikupaswa kuwa jinai bali
ya madai.
Akisoma hukumu hiyo, saa tano asubuhi, Dudu alisema upande wa Jamhuri
uliokuwa ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali, Charles Anindo, katika
harakati zake za kutaka kuthibitisha kesi yake ulileta mashahidi watano
wakati upande wa washitakiwa waliokuwa wanatetewa na wakili wa
kujtegemea, Alex Mshumbusi, ulileta mashahidi wanne, ambao ni
washitakiwa wenyewe na shahidi mmoja.
No comments:
Post a Comment