Kipindi cha FAMILIA 3 kutoka Jamii Production
Mtayarishaji
na Mtangazaji wa kipindi cha FAMILIA, Georgina Lema akiwa na mgeni wake
Mayor Mlima ndani ya studjio wakati wa kipindi.
Pale familia zinapoamua kusonga mbele na maisha yanayohusisha watu zaidi ya waliokuwepo awali, mambo mengi hutokea. Kuna wakati ambao watoto huonekana kutokuwa tayari kupokea ujio wa watu wengine kwa kudhani watapoteza sehemu ya hadhi yao ndani ya nyumba (ama unaweza kusema wanakuwa na namna fulani ya wivu)
Pale familia zinapoamua kusonga mbele na maisha yanayohusisha watu zaidi ya waliokuwepo awali, mambo mengi hutokea. Kuna wakati ambao watoto huonekana kutokuwa tayari kupokea ujio wa watu wengine kwa kudhani watapoteza sehemu ya hadhi yao ndani ya nyumba (ama unaweza kusema wanakuwa na namna fulani ya wivu)
Lakini
pia, hata wazazi wanaoingia katika maisha ya familia nyingine hushindwa
kurekebisha mwenendo wao kuweza kuwafaa watoto wanaowakuta na matokeo
yake kuleta namna ya kutoelewana baina yao.
Tunaweza
kuangalia sababu mbalimbali zinazosababisha haya, na kunaweza kuwa na
sababu nyingi zaidi ya tunazoweza kufikiria juu ya hili, lakini
tunaamini kuwa yapo mambo ambayo kama tutayazingatia, yanaweza kutupa
mwanga wa kuepuka hili.
Georgina Lema akiendesha kipindi. Pembeni ni "fundi mitambo" wake Mubelwa Bandio
Karibu
katika kipindi hiki cha FAMILIA kutoka Jamii Production kinachokujia
kila Jumatatu, ambapo katika kipindi hiki, tumeanza na sehemu ya kwanza
ya mfululizo wa vipindi vyetu vitakavyozungumzia changamoto za FAMILIA
ZA KUFIKIA.
Yaani, kuwa mzazi wa kufikia, ama wengine wanasema MZAZI WA KAMBO.
Je! Ilikuwaje zamani? Ikoje sasa na kubwa zaidi tutajaribu kuangalia...Je! ilistahili kuwaje?
Katika kujadili hili, tumeungana na wazazi kujadili mada hii, na pia kusoma makala za uchunguzi juu ya hili.
Georgina Lema akijadiliana jambo na msimamizi wa kipindi chake Abou Shatry kuhakikisha kila kitu kiko sawa kabla ya kipindi.
Twawapenda...Tukutane juma lijalo katika muendelezo wa kipindi hiki kuhusu FAMILIA ZA KUFIKIA / FAMILIA ZA KAMBO
No comments:
Post a Comment