HOT NEWS: SUGU NA MWANJELWA WADAIWA KUGOMBANISHWA
*Nia ni
kubadili ajenda ya maendeleo ili yawe malumbano
Na Gordon
Kalulunga, Mbeya
KAULI
iliyoandikwa hivi karibuni kuwa Waziri wa Maendeleo Jinsia na watoto, Sophia
Simba kwamba Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ana mapepo, imeelezwa kuwa
imelenga kubadili ajenda ya maendeleo katika Jiji la Mbeya na kuwaingiza katika
malumbano Mbunge huyo na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary
Mwanjelwa.
Hayo
yameelezwa na wananchi na baadhi ya wanasiasa waliokuwepo eneo la mkutano na
kwamba kauli hiyo haikutolewa na viongozi hao bali ilitolewa na Mjumbe wa
Mkutano mkuu wa Taifa kupitia wilaya ya Mbeya mjini, Charles Mwakipesile.
Mwakipesile,
ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari, katika mkutano wa Sophia Simba,
alisema Mbunge Joseph Mbilinyi(Sugu), alipagawa na pepo wachafu ndiyo maana
aliingilia ugomvi ambao haukumhusu na kuamua kupigana wakati muhusika(Freeman
Mbowe) hakukataa kutoka nje.
‘’Kwasababu
yeye hana hoja na alikuwa amekosa cha kuzunguza kuhusu mswada wa katiba, hivyo
aliona ili aonekane kwenye luninga ni vema akaingilia suala ambalo halikumhusu
maana katika jimbo lake ameshindwa kutekeleza ahadi ya kujenga mabwawa ya
samaki katika kata 36 za Jiji la Mbeya kama alivyowaahidi wananchi’’ alisema
Mwakipesile.
Walisema
kuwa inashangaza kuona baadhi ya waandishi wa habari kuamua kwa makusudi
kutumika na kuhamisha maneno ya Mwakipesile na kumlisha Dr. Mwanjelwa ambaye
hakugusia wala kuunga mkono kauli hiyo iliyoelekezwa kwa Mbunge Sugu.
Akihojiwa na
Mtandao huu wa www.kalulunga.blogspot.com Dr.
Mary Mwanjelwa alisema kuwa amechafuliwa lakini ni vema jamii ikaelewa kuwa
sera yake yeye siyo kulumbana bali ni kufanya kazi na kutekeleza ilani y chama
chake (CCM).
‘’Walioandika
kitu ambacho sikukisema mimi hawajanitendea haki, wanataka kunigombanisha bure
na mbunge mwenzangu na huu ni uchochezi, lakini siwezi kurudi nyuma kuwatumikia
kimaendeleo wananchi wa Jiji la Mbeya na mkoa kwa ujumla’’ alisema Mwanjelwa.
Hayo
yamekuja baada ya siku mbili baada ya Waziri Sophia Simba ana Mbunge huyo
kudaiwa kumkejeli Sugu, kuwa awapo bungeni anaongozwa na mapepo wakati Sugu
anasema anayoyafanya yote yana Baraka kutoka kwa wananchi wa jimbo lake la
Mbeya Mjini.
No comments:
Post a Comment