Dkt. Fenella Mukangara atembelea Maonyesho ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere leo mjini Iringa.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (koti
jeusi) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Sihaba Nkinga wakitembelea
banda la maonyesho la wajasiriamali kutoka wilayani Bagamoyo
wanaoshiriki maonesho ya Wiki ya Vijana mkoani Iringa.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (mwenye
mavazi meusi) akiwasili katika viwanja vya maonyesho ya Wiki ya Vijana
Shule ya Msingi Mlandege, Iringa akiwa ameambatana na viongozi wengine
wa Wizara hiyo Katibu Mkuu Bi. Sihaba Nkinga (wa tatu kutoka kulia),
Naibu Katibu Mkuu Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto),Mkurugenzi wa
Utamaduni Prof. Herman Mwansoko (kulia) na Mkurugenzi wa Vijana James
Kajugusi (wa pili kulia).
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa leo mara baada ya
kuangalia maandalizi ya sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge katika
Uwanja wa Samora mkoani Iringa. Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.
atibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi.Sihaba
Nkinga(kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Kutengeneza bidhaa mbalimbali za asili zikiwemo sabuni za kuogea ya
MKIPI yenye Makao yake Pemba na Zanzibar Bw. Mohamed Foum wakati
alipotembelea banda la maonyesho la kampuni hiyo leo.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
(kushoto) akitembelea banda la Maonyesho ya kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere leo mjini Iringa.





No comments:
Post a Comment