AIRTEL YATOSHA BABA LAO YATANUA KIFUA ZAIDI TENA
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Bw. Levi Nyakundi akitangaza rasmi
kuboreshwa kwa huduma ya Airtel Yatosha Baba lao baada ya kuongeza
dakika zaidi, MB za intaneti zaidi na SMS bila kikomo kwa bei ileile
ya 999 kwa siku wakati wa hafla fupi maalum iliyofanyika leo makao
makuu ya Airtel Dar es salaam.
dakika zaidi, MB za intaneti zaidi na SMS bila kikomo kwa bei ileile
ya 999 kwa siku wakati wa hafla fupi maalum iliyofanyika leo makao
makuu ya Airtel Dar es salaam.
======= ===== =======
Airtel Yatosha Baba lao yazidi kutanua kifua
* Kwa beil ile ile ya shilingi 999 unapata SMS bila kikomo,
dakika 55 na MB 500 kuperuzi mitandao upendavyo
Airtel Tanzania kupitia vifurushi vyake vya Yatosha imeendelea
kujiimarisha zaidi ikiwa ni siku chache tangu kumalizika kwa
promosheni yake kabambe ya shinda nyumba 3.
Akiongea kuhusiana na BABA LAO ilivyozidi kufunguka kwa kuboreshwa
zaidi Mkurugenzi wa Masko wa Airtel Tanzania Levi Nyakundi alisema
"Airtel Yatosha baba lao imenogeshwa zaidi tena! Tunasema yaani Ni
Airtel yatosha ni Baba lao na bado itaendelea kubakia hivyo, kwa sasa
kwa shilingi 999 tu mteja atapa SMS bila kikomo kwenda mtandao wowote,
MB 400 za kuperuzi intanet na pia atapata dakika 55 zakupiga simu
kwenda mtandao wowote nchini.
Ikumbukwe kuwa vifurushi vyote vya siku vya yatosha vinadumu kwa
masaa 25 tangu mteja anapojiunga hii ni kwa lengo maalum kabisa
kumfanya mteja wetu yeyote aweze kufurahia thamani ya pesa yake katika
huduma zetu.
Lengo letu ni kuona Huduma yetu ya Airtel yatosha baba lao inaendelea
kuwafaidisha watanzania kuendelea kuokoa pesa nyingi zaidi walizokuwa
wakitumia kwenye mawasiliano na kuanza kuzitumia katika shughuli
nyingine za uchumi wa taifa na jamii kwa ujumla.
Kujiunga na kifurushi chochote cha SIKU, WIKI au MWEZI piga *149*99#
Nae meneja Masoko wa Airtel Bi, Anethy Muga alisema "Ikiwa utajiunga
na vifurushi hivi vilivyoongezewa muda na dakika ni hakika kabisa kuwa
utaokoa pesa nyingi na utaweza kujiweka katika nafasi nzuri sana
yakupanga mambo mengi ya kiuchumi kwa kuwa unaokoa pesa nyingi"
Airtel yatosha inaendelea na mkakati wa kutosha zaidi kumtimizia
mtanzania haki yake ya mawasiliano kwa kumpa mawasiliano nafuu huku
Airtel pia ikihakikisha mawasiliano madhubuti yanapatikana alieleza
Bi, Muga.
Promosheni ya Airtel yatosha sjhinda nyumba 3 ilikwisha mwanzoni mwa
wiki hii, laikini bado huduma ya yatosha inaendea na sasa vifurushi
vya huduma hiyo vimeongewa zaidi kwa lengo la kuifanya huduma hiyo
kuwanufaisha wateja zaidi.
No comments:
Post a Comment