MAZALA AWATAKA WAFANYABIASHARA WA NGAZI ZOTE MKOANI SINGIDA KUJIUNGA NA CCM ILI KUPATA MAFANIKIO

Mfanyabiashara maarufu mjini Singida,
Mushi Kimboka (aliyweshika maiki) akitoa taarifa yake kwa mjumbe wa
halmashauri kuu CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida, Hassan
Mazala(aliyevaa miwani) juu ya ujenzi wake wa hotel ya Chemuchemu Park
iliyoko katika kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji wa Singida.
Mkurugenzi mtendaji wa hotel ya
kitalii ya Stanley Motel, Eward Malya maarufu kwa jina la Hali Ngumu
akitoa nasaha zake kwenye hafla ya uzinduzi wa hotel ya Chemuchemu park
iliyopo kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji wa Singida.Hali Ngumu
amewataka wafanyabiashara kufanya biashara halali kwa bidii na kisha
wabane matumizi kwa madai kuwa 'hali ni ngumu'.
Mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC)
taifa manispaa ya Singida,Hassan Mazala akizindua rasmi hotel ya
Chemuchemu Park iliyopo katika kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji
wa Singida.
Wanachama wapya wa CCM baada ya
kukabidhiwa kadi juzi na mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa
Hassan Mazala (hayupo kwenye picha).
Kikundi cha burudani cha kijiji cha
Manguanjuki kikitoa burudani wakati wa uzinduzi wa shina la wakereketwa
wa CCM katika hotel ya Chemuchemu park.
Mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC)
taifa manispaa ya Singida,Hassan Mazala (wa tano kushoto mbele) akiwa
kwenye picha ya pamoja na wadau waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa hotel
ya Chemuchemu park iliypo kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji wa
Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM
(NEC) taifa manispaa ya Singida Hassan Mazala, amewahimiza
wafanyabiashara wa ngazi zote kujiunga na CCM, kwa madai kuwa ni chama
pekee kinachowajengea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao kwa amani
na utulivu.
Mazala ametoa wito huo muda mfupi
baada ya kuzindua tawi la wakereketwa wa hotel mpya na ya kisasa ya
Chemuchemu Park, iliyopo katika kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji
wa Singida.
Amesema uzoefu unaonyesha wazi
kwamba wafanyabiashara wamekuwa wakishirikiana na CCM kwa muda mrefu na
hali hiyo inapaswa kuendelezwa kwa sababu inazinufaisha pande zote
mbili.
Akifafanua zaidi amesema amani na
utulivu ndio inayopelekea wafanyabiashara na Watanzania wengine wote,
wafanye shughuli zao halali kwa uhuru mpana zaidi na ambao hauathiri
sheria zilizowekwa.
MNEC huyo amesema CHADEMA inaonyesha
ilani yake ni kupandikiza chuki, hasira, kuchonganisha watu na
upotoshaji uliopitiliza, na kwa hali hiyo, CHADEMA sio mahali rafiki kwa
wafanyabiashara.
Katika hatua nyingine, Mazala
ametumia fursa hiyo kuwahimiza viongozi/watendaji wa CCM na wa serikali
yake, kuwa karibu na wafanyabiashara ili kujua matatizo/kero
wanazokabiliana nazo na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Kwa
upande wa wafanyabiashara, amewataka wafanye kazi halali kwa bidii na
kwa ubunifu mkubwa na kuhakikisha wanabana matumizi au wawe na nidhamu
ya matumizi.
No comments:
Post a Comment