RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AWAONGOZA WATANZANIA MAADHIMISHO YA MIAKA 49 YA MUUNGANO UWANJA WA UHURU LEO
Rais wa
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dk. Jakaya Mrisho
Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama lililoandaliwa
maalum kwa ajili maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es salaam
na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya Siasa na
Mabalozi pamoja na wageni waalikwa mbalimbali ili kushuhudia maadhimisho
hayo.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-UWANJA WA UHURU)
R
Rais Dk. Jakaya Kikwete akielekea jukwaani mara baada ya kukagua gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama katika maadhimisho hayo
Rais Dk.
Jakaya Kikwete akiwa jukwaani pamoja na viongozi wengine kutoka kulia
ni Rais Mstaafu Benjamin Wiliam Mkapa, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. Gharib Bilal, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na
Kutoka kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Rais Wa Zanzibar Dk. Ali
Mohamed Shein.
Rais Wa
Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kulia akiwa na viongozi wengine katika
jukwaa kuu kutoka kushoto ni Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa
pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Idd, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na
Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete
akiingia uwanjani katika gari maalum huku akisindikizwa na Mkuu wa
Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya
Kikwete akiwapungia mkono wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo
kwenye uwanja wa Uhuru
Kikosi cha Jeshi la Ulinzi JWTZ wanamaji kikipita na kutoa heshima mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete .
Kikosi cha Jeshi la Kujenga taifa JKT kikitoa heshima mbelea ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete.
Kikosi cha Jeshi la Kujenga taifa JKT kikitoa heshima mbelea ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete.
Kikosi Maalum Cha Bendera kikitoa heshima zake bele ya Rais Jakaya Kikwete Kikosi chamJeshi la Ulinzi JWTZ nchi kavu kikipita na kutoa heshima mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete.
Watoto
wa halaiki wakionyesha ujumbe mbalimbali kuhusu Muungano wetu mbele ya
Rais Jakaya Kikwete na maelfu ya Watanzania waliohudhuria katika
maadhimisho hayoPICHA ZOTE KWA HISANI YA FULLSHANGWE BLOG

No comments:
Post a Comment