JK AZINDUA MIRADI MIWILI MIKUBWA WILAYANI IGUNGA LEO
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa daraja la kisasa katika eneo la Mbutu,Wilayani Igunga leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akizindua mradi wa Chujio la maji safi kwa mji wa Igunga sehemu za
Bulenya ambapo wakazi zaidi ya asilimia 70 wa mji huo watapata maji
safi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiangalia mashine ya kuchimbia mashimo ya nguzo za daraja kabla ya
kwenda kukata utepe kwa kuashiria kuzindua ujenzi daraja la
Mbutu,Wilayani Igunga leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tanroads,Eng. Patrick Mfugale (alieshika maiki) akumuonyesha Rais Kikwete ramani ya Mradi wa Ujenzi wa daraja la kisasa katika eneo la Mbutu,Wilayani Igunga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiongea na kutoa ushauri kwa kundi la vijana 10 ambao baada ya
kumaliza chuo kikuu wamejikusanya na kuunda kikundi cha ujasiriamali
mjini Igunga wakijishugulisha na Kilimo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akikagua sehemu ya vyanzo vya mradi mpya wa maji safi kwa mji wa Igunga
sehemu za Bulenya ambapo wakazi asilimia 70 wa mji huo watapata maji
safi
Wananchi wakivuka katika sehemu
itayojengwa daraja la kisasa eneo la Mbutu,Igunga Mkoani Tabora ambao
ujenzi wake umezinduliwa leo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete, hatua
ambayo itatatua kabisa tatizo la miundombinu.PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment