Waziri Mukangara awatembelea vijana na saccos zilizonufaika na fedha za mkopo wa mfuko wa vijana mkoa wa Mwanza
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akiongea jambo na Mkurugenzi
Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo Vijana James Kajugusi (aliyevaa
suti ya blue) jana mara baada ya kumaliza kuwatembelea vijana
wajasiriamali wa soko kuu la jijini Mwanza ambao walipata mkopo kutoka
mfuko wa vijana kupitia Halmashauri ya jiji. Waziri Dk. Mukangara
aliwatembelea wajasiliamali hao ili kuona fedha walizopata
zimewasaidiaje kama kundi la vijana na kijana mmojammoja.
Mwenyekiti wa SACCOS ya
Wafanyabiashara Wadogowadogo Mkoa wa Mwanza (WADOKI) Mussa Ally
akimuonyesha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella
Mukangara (kulia) mfano wa jengo wanalolitarajia kujenga hivi karibuni
kama kitega uchumi chao jana jijini Mwanza. SACCOS hiyo ilipata mkopo
kutoka mfuko wa vijana mwaka 2009 fedha ambazo waliwakopesha vijana
wanachama 12.


Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akiongea jambo na
Songaleli Mzee (kulia) ambaye ni mfanyabiashara wa soko kuu la jijini
Mwanza aliyepata mkopo kutoka mfuko wa vijana na kufanya biashara ya
nafaka. Katikati ni Edward Kabululu ambaye ni Mwenyekiti wa Mwanza
SACCOS ambayo ni moja kati ya 14 za mkoa wa Mwanza zilipata fedha za
vijana mwaka 2009 na kumpatia mkopo Mzee.
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (katikati) akiongea na
wafanyakazi wa SACCOS ya Wafanyabiashara Wadogowadogo Mkoa wa Mwanza
(WADOKI) jana jijini Mwanza juu ya umuhimu wa kuwahimiza wanachama wao
hasa vijana kuitumia mikopo wanayoipata katika shughuli za kilimo cha
chakula, ufugaji wa samaki na uvuvi ili kuisaidia nchi kuepukana na
tatizo la njaa. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo
ya Vijana James Kajugusi na kushoto ni Mwenyekiti WADOKI SACCOS Mussa
Ally.
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kulia) akimuangalia mteja
akisukwa nywele katika Saluni ya Juvee Kanuzile (hayupo pichani) ambaye
alipata mkopo kutoka mfuko wa vijana kupitia halmashauri ya jiji mwaka
2009 na kufanya biashara ya saluni. Waziri Dk. Mukangara alitembelea
saluni hiyo ili kuona fedha alizopata Kanuzile zimemsaidiaje kama
kijana.
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (katikati) akimsikiliza
Jummanne Izengo (kulia) ambaye alimueleza jinsi alivyonufaika na mkopo
alioupata kutoka mfuko wa vijana ambao umemuwezesha kununua mashine ya
kusaga nafaka, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Vijana
James Kajugusi . Waziri Dk. Mukangara alimtembelea Izengo jana katika
eneo lake la biashara lililopo Mwaloni jijini Mwanza ili kuona fedha
alizopata zimemsaidiaje kama kijana.Picha na Anna Nkinda – Maelezo.
No comments:
Post a Comment