Header Ads

Redknapp kufanyiwa upasuaji wa moyo

Redknapp kufanyiwa upasuaji wa moyo

Klabu ya Tottenham imetibitisha meneja wake Harry Redknapp atafanyiwa upasuaji mdogo wa moyo siku ya Jumatano.

Redknapp ambaye ana umri wa miaka 64 alilazwa hospitali siku ya Jumanne usiku kwa ajili ya vipimo na atafanyiwa upasuaji huo katika mrija mdogo wa damu.

Redknapp hakuweza kusafiri na kikosi cha timu yake kilichopo Urusi kwa ajili ya pambano la Ligi ya Europa dhidi ya timu ya Rubin Kazan siku ya Alhamisi.

Spurs wanaogoza katika kundi lao la A, wakiwa mbele kwa pointi mbili dhidi ya timu ya PAOK ya Ugiriki.

Meneja msaidizi Kevin Bond na kocha wa kikosi cha kwanza Joe Jordan watakamata nafasi ya Redknapp.

Haijulikani ni kwa muda gani Redknapp hataweza kufanya kazi, ingawa mengi zaidi yatafahamika baadae siku ya Jumatano katika mkutano wa waandishi wa habari utakaoitishwa na klabu hiyo huko Urusi.

Redknapp siku ya Jumatano aliliambia gazeti la the Sun ana matumaini tatizo lake la afya halitamsumbua kusimamia mechi ya Jumapili ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Fulham.

Amesema: "Natumai naweza kurejea kazini katika siku chache zijazo."

No comments:

Powered by Blogger.