
KIONGOZI HUYU AMBAYE AMECHAGULIWA TENA KUENDELEZA LIBENEKE HILO.
Zuriki,
Uswizi - 01/06/2011. Wajumbe wa shirikisho la soka duniani
FIFA,wamemchagua tena rais wa shirikisho hilo kushikiria kiti hicho kwa
kipindi kingine cha miaka minne.
Wajumbe hao waliweza kumchagua Sepp Blatter kwa wingi wa kura zipatazo 186 kati ya kura 203 zilizo pigwa.
Sepp
Blatter, ambaye alikuwa mgombea pekee katika kiti hicho, baada ya
mpinzani wake Mohamed bin Hammam kujitoa kutokana na kashfa za rushwa.
Hata
hivyo, uchaguzi huo ulifanyika baada ya Uingereza kushindwa
kuwashawishi nchi wanachama wa shirikisho hilo kupiga kura ya kutaka
uchaguzi huo usimamishwe kwa muda, ili achaguliwe mpinzani dhidi ya
Sepp Blatter, lakini matokea ya kura hizo yalipinga maombi ya Uingereza
kwa 172 kutaka uchaguzi ufanyike na 17 kuunga mkono Uingereza.
Kuchaguliwa
kwa Sepp Blatter, kumeaandamana na misukosuko mingi iliyo ikuta
shirikosho hilo baada ya kashfa za rushwa kuandama uongozi mzima wa
shirikisho hilo FIFA.
Akiongea
baada ya matokeo ya uchaguzi, rais huyo wa FIFA Sepp Blatter alisema
"Mimi ni kaptain ambaye naongoza jahazi lililo kumbwa na mawimbi na tuta
hakikisha shirikisho la soka litakuwa mairi na kulinda heshima ya
mchezo huu, kuweka wazi kila jambo na kuhakikisha matatizo yaliyo tokea
hayatotokea tena, na nahaidi kwa baraka za Muumba na uzima atakao nipa
basi tuta fanikiwa kuhakikisha shirikisho hili lina kuwa swafi na
imara."
No comments:
Post a Comment