BREAKING NEWS: WANAFUNZI WA UDOM WAJIANDAA KUGOMA
Baadhi ya wanafunzi wa kitivo cha sayansi ya jamii wakiwa katika
makundi makundi wakijadili suala la mafunzo kwa vitendo mara baada ya
kubandikiwa tangazo ambalo linasema kuwa Hakuna mafunzo Kwa Vitendo
Wanafunzi Wa Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii, Sanaa na Lugha wakisoma
tangazo lililoandika kuwa hakuna mafunzo kwa vitendo lililobandikwa huku
wengine wakijadili kiunagaunaga.
Wanafunzi Wakimsikiliza kwa makini raisi wa kitivo cha sayansi ya
jamii, sanaa na lugha Mh Mwakibinga Philipo Wakati akitoa Ufafanunuzi Na
jinsi Serikali ya wanafunzi itakavyofanya kuhusiana na tatizo hilo
Raisi Wa Kitivo Cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha Akitoa maelezo kuhusiana na tangazo hilo linalosema kuwa hakuna field
Mnamo tarehe 20 disemba mwaka 2010 Wanafunzi Wa Kitivo cha Sayaynsi
ya jamii sanaa na Lugha Waligoma kuingia madarasani Kwaajili ya
kushinikiza kupewa mafunzo ya vitendo ambayo ni haki ya kila mwanafunzi
wa elimu ya juu hali iliyopelekewa kutokea kwa ghasi aambazo polisi wa
kutuliza ghasia walitumia nguvu pamoja na mabomu ya machozi ili kutuliza
hali iliyochafuka kipindi hiko.
Mgomo huo ulidumu kwa suku mbili mfululizo hadi kupelekea Waziri Wa
Elimu Shukuru Kawambwa na Mwenyekiti Wa Bodi Ya Chuo Kikuu Cha Dodoma na
Waziri Wa Mambo Ya Ndani Wa Nchi Mh Shamsi Vuai Nahodha Kufika Chuo
Hapo Siku Ya Tatu na kuahidi Kulitafutia ufumbuzi na Kuwahidi wanafunzi
hao kuwa watakwenda kufanya mafunzo kwa vitendo na kuuagiza Uongozi wa
chuo Kuwatafutia Wanafunzi sehemu ya Kufanyia Mafunzo Kwa Vitendo.
Mara Baada ya Muda Kupita Chuo Kilianza Mpango Mzima Wa KUwatafutia
Wanafunzi Sehemu Za Kufania Mafunzo Kwa Vitendo Na Kwa Kiasi kikubwa
Wanafunzi Wengi waliweza Kupata nafasi hizo kwaajili ya kufanya mafunzo
kwa vitendo katika kipindi Cha likizo huku wanafunzi wakionyesha
wasiwasi wasiwasi wa kupata fedha zao za mafunzo kwa vitendo kitu
ambacho Raisi Wa Kitivo Mh Mwakibinga Akasisitiza Kuwa Hawataingia
Katika Mitihani ya Muhula Wa Mwisho bila Fedha kuingia katika akaunti
zao kitu ambacho raisi wa kitivo hiko aliweza kukifuatilia na kuonyesha
dalili za kuzaa matunda.
kwa habari zaidi bofya hapa











No comments:
Post a Comment