CHINA inakaribia kuipiku Marekani kwa ukubwa wa masuala ya kisayansi pengine ifikapo mwaka 2013, mapema kuliko ilivyotabiriwa awali.
Hilo lilikuwa sehemu ya hitimisho la ripoti ya utafiti mpya mkubwa uliofanywa na Royal Society, Taasisi ya Taifa ya Sayansi ya Uingereza.
Wachambuzi waliochapisha utafiti huo moja ya tafiti muhimu za kisayansi wamebainisha ukuaji wa nyanja ya sayansi ya China.
Utafiti huo, Ujuzi, Mitandao na Mataifa, unaelezea changamoto zinazozikabili zile zilizojulikana kama ‘tamaduni za sayansi’ duniani; Marekani, Ulaya na Japan.
Takwimu hizo zinatokana na ripoti zilizochapishwa na majarida ya kimataifa yanayotambulika na kuheshimika.
Mwaka 1996, ukiwa ni mwaka wa kwanza wa uchambuzi Marekani ilichapisha ripoti 292,513 zikiwa zaidi ya 10 ya za China ambazo zilikuwa 25,474.
Kufikia mwaka 2008, ripoti za tafiti za Marekani ziliongezeka kidogo kufikia 316,317 lakini za China zikiongezeka mara saba kufikia 184,080.
Makadirio ya awali ya mpanuko wa sayansi ya China ulikadiria kwamba China ingeipiku Marekani baada ya mwaka 2020.
Lakini utafiti huo unaonyesha baada ya China kuipiku Uingereza kama mzalishaji namba mbili wa tafiti duniani itaipiku Marekani kipindi cha miaka kama miwili ijayo
No comments:
Post a Comment