Header Ads

RUSHWA
Rushwa ni kitendo cha kupokea au kutoa kitu ambacho si halali kwa kuhonga au kuhongwa neno rushwa limekuwa na uzito mkubwa katika nchi yetu na hata dunia.
serikali imejitahidi sana kupita vita suala la rushwa lakini kwa kiasi fulani watu wamejaribu kujirekebisha au kupiga hatua furani.Tumeona viongozi wetu wa uma wamefikishwa katika vyombo vya sheria kwa makosa ya rushwa.Watanzania wanalia kila kukicha kwa baadhi ya wachache wanaoendesha mchezo huu mchafu wa kuendeleza suala hili la rushwa ambalo limesababisha mali za umma kuuzwa kwa kinyemela au kutumia madaraka vibaya.Tatizo la rushwa nchi limetokana na utawala mmbovu ambao umewekwa na viongozi wenye tamaa na wasio waadilifu na wasio mwogopa mungu kwa kufanya mambo yasiyompendeza mungu na watanzania kwa ujumla.Ningeiomba serikali iiweze kutunga sheria kali ambazo zitawabana watu wanaoendeleza suala hili la rushwa.Tukiweza kufuata sheria hizi basi wote wanaopokea na kutoa rushwa wataogopa kwani watajua sheria itawabana.Kutokana na katiba yetu ilivyo na mapungufu tunaona viongozi wetu wa ngazi za juu wanashindikana kubanwa kutokana na sheria hizi mbovu zinawalinda.Tunaona hata mkuu wa pccb angekuwa chini ya bunge ili kumwondolea kinga ya kuogopa kutoa taarifa za viongozi wa ngazi za juu yaani kwa sahihi kwani rais hataweza kumtoa bila idhini ya bunge.Tumeona nchi kama china wamejaribu kutunga sheria kali kudhibiti mwanya wa rushwa kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kutunga sheria zao kali na zinawabana wabana wachache hawa ambao wanajaribu kuvunja sheria za nchi kwa makusudi.
Mimi kama denis nasema rushwa haikubaliki ndani ya nchi hii tumewachoka wanaoendeleza mchezo huo ambao unasababisha watanzania wengi wanaishi kama yatima kwa kukosa matumaini kwani rushwa imekuwa kama msiba ndani ya nchi hii.Tukishirikiana kwa pamoja kupiga na suala hili naimani rushwa itaisha tu na kufikia malengo.Ningeliomba bunge pamoja na taasisi zote ziwe mstari wa mbele katika kukemea rushwa na kusema rushwa haikubaliki.
Rushwa imegawnyika katika makundi mengi leo ukienda mahospitalini,mahakamani,msikitini,kwenye vyombo vya dola,vyombo vya habari na elimu tunaona rushwa.Rushwa si kwa serikali tu bali imesambaa kila idara tumeona mambo mengi yanaenda ovyo kutokana hali hiyo kuwa mzizi ambao watu wachache wanaendeleza tabia hii.
Ushauri wangu kama denis hendry nasema ili iweze kuisha ni lazima kila mtanzania aweze kukataa kupokea au kutoa kwani hata kupokea shilingi mbili kwa kitu ambacho si halali au halali hiyo ni rushwa.Serikali iweze kutoa elimu inayohusu rushwa katika mashule yetu kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu ili watoto waweze kujua madhara ya rushwa na kukataa tangu wakiwa shule ya msingi ili tuwe na kizazi kisichopenda rushwa.Pamoja na kuwatumia viongozi wetu wa dini waweze kuhamasisha wafuasi wao kuchukia rushwa na kukataa kwa kufuata vitabu vyao vitakatifu.Mimi naona njia hizi tatu ambazo ni viongozi wa dini kuhamasisha,elimu ya rushwa kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu.pamoja na sheria kali kutungwa.Tukiweza kuweka vitu hivi vitatu tutakuwa tumetokomeza rushwa naimani itakwisha kabisa

"nasema rushwa haikubaliki" "nasema rushwa haikubaliki"
" mungu ibariki tanzania"
" mungu ibariki afrika"
asanteni sana.
DENIS HENDRY MALAMSHA
SIMU NAMBA:- 0712-550508
0765-002472
e-mail:crispaseve@gmail.com

1 comment:

mjasiliamali said...

angalia wasikuzime kama taa

Powered by Blogger.